Kwa Wakristu ni muhimu kuheshimu tofauti za kilitujia zilizopo- AskofuMkuu Martin
aeleza.
(Vatican Radio) Kwa jinsi gani nguvu na uhai wa yatokanayo na mkutano wa 10 wa Baraza
la Makanisa Ulimwenguni, vinaweza kuleta msukumo mpya katika harakati za kiekumeni
? Na kwa jinsi gani Wakristo wa madhehebu mbalimbali wanaweza kugundua upya asili
ya mizizi yao ya kiroho kwa pamoja? Na jinsi viongozi Katoliki wanalenga kutekeleza
malengo ya Mkutano huu wa 10 wa WCC ndani ya maisha ya Makanisa yao ?
Ni maswali
yaliyotolewa na Philippa Hitchen kwa Askofu Mkuu wa Dublin, Diarmuid Martin, mjumbe
Katoliki katika mkutano wa 10 wa WCC, na Mratibu mwenza aliyemaliza muda wake wa
kuwa mjumbe katika utume wa pamoja katika Kazi za Kanisa Katoliki kwenye Baraza
la Makanisa Ulimwenguni. Askofu Mkuu Martin alijibu maswali na maeelzo kwamba,
kati ya yote kwake yeye maazimio yaliyotolewa juu ya vijana ,yanayo himiza kutunza
mizizi ya kiroho ya kiekumene inaonyesha kwamba, kwa kadri Wakristu wanavyo elewa
utendaji wa kufanana wa watakatifu, katika maisha yao ya kawaida ndivyo twanavyo zidi
kukaribiana katika misingi ya kiekumeni. Na kwa jinsi hiyo, kwa kutazama Maadiko
ya Kiliturujia , nyimbo na maandiko ya Kikristo, kabla ya mgawanyiko wa Wakristu,
mna onekana vile vinavyo waunganisha pamoja Wakristu , ingawa kwa kwa bahati mbaya
, ameonya, muda wa kutosha hautolewa katika kuyatazama hayo kwa makini zaidi. Askofu
Mkuu Diarmuid anasema baada ya mkutano huu, ujumbe anaopeleka nyumbani kama Askofu
wa jimbo , ni kuhakikisha uzoefu alioupata katika mkutano huu, anaushirikisha pia
kwa jimbo lake, kwenye maisha ya siku hadi siku ya Kikristo Jimboni mwake na pia
katika nchi nyingine .... Anaendelea kueleza kwamba, uzoefu wa wa Mkutano huu
kwenye ngazi ya kibinadamu na kiroho, ni maajabu.Umekuwa ni kati ya mikutano michache
sana ya aina hii iliyowahi kufanyika duniani kwa Wakristu kuuishi mchanganyiko huu
kwa maelewano ya kujiona wao ni kundi moja linaloongozwa na Mchungaji mmoja Kristu.
Na hivyo anaona kwamba, umoja Wakristu haupaswi kuishia katika umoja na mshikamano
wa kufanana katika kila jambo, lakini hatima yake inapaswa kuhakikisha utofauti wa
utendaji wa kiliturujia unaheshimiwa katika maisha ya Kanisa zima...
Na kwamba,
kuna nguvu fulani katika Mkutano huu, mengi yakitokana na ukweli kwamba, vijana
wameshirikishwa katika mkutano huu. Na hivyo amebaki akijuìiuliza kama inafaa pia,
kwa mfano katika mkutano ya Sinodi ya Maaskofu Katoliki , kuwa na uwezekano wa kuwa
na mchanganyijko wa aina hii , kuishirikisha pia furaha hii ya vijana , na hata uhuru
wa kuwa wachokozi tu, katika baadhi ya changamoto zinazo pambanisha Kanisa . Kwake
yeye anadhani pia hilo ni muhimu.