Tanzia: Kardinali Domenico Bartolucci amefariki dunia
Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Domenico Bartollucci kilichotokea mapema
Asubuhi Jumatatu hii 11. 11 2013. Kardinali amefikwa na mauti akiwa na umri wa miaka
96. Kwa kifo chake, Idadi ya Makardinali imebaki 200, ambamo kati yao wenye haki
ya kikatiba kupiga kura ni 109 na wasiokuwa na haki ya kupiga kura ni 91. Marehemu
kwa muda wa miaka mingi alikuwa ni Mkurugenzi wa Muziki Mtakatifu wa Kipapa katika
kanisa ldo la Sistini ndani ya Vatican. Alifanywa kuwa Kardinali na Papa Benedikto
XV1, wakati wa kikao cha Makardinali "Consistory" tarehe 20 Novemba 2010. Mara
baada ya taarifa ya kifo kumfikia Papa Francisko , mara aliandika na kutuma salaam
zake za rambirambi kwa ndugu wa Marehemu Sandro na Stefano Bartolucci , na kwa jumuiya
ya Jimbo la Fiorentina pamoja na wote waliouguwa kwa namna moja au nyingine na katika
maombolezo haya. Papa ametaja sifa za Marehemu kwamba alikuwa ni mtunzi maarufu
na mwanamuziki aliyeyatolea maisha yake yote kwa ajili ya Muziki Mtakatifu, akionyesha
utahabiti wa imani yake kwa Kristu. Papa ametoa shukrani kwa matunda yake kama Mkurugenzi
wa Sistine Chapel, na hekima zake, katika upigaji wa muziki wa kumsifu Mungu. Papa
ameeleza na kusali kwa maombezi ya Bikira Maria, kusmpokea mtumishi huyu wa Mungu
katika makao ya milele.