2013-11-09 15:00:27

Papa aguswa na mahangaiko ya wananchi wa Ufilippini


Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko na majonzi makuu taarifa za mahangaiko ya wananchi wengi wa Ufilippini kutokana na kukumbwa na kimbunga ambacho kimesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujiunga naye kwa ajili ya kuwaombea waathirika wa kimbunga hiki nchini Ufilippini.







All the contents on this site are copyrighted ©.