Serikali ya Chad na Vatican watiliana sahihi mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya ujenzi
wa Jamii inayosimikwa katika misingi ya haki na amani
Vatican na Serikali ya Chad, tarehe 6 Novemba 2013 wametiliana sahihi mkataba unaoliwezesha
Kanisa nchini Chad kutambulika kisheria. Ujumbe wa Vatican katika makubaliano haya
umeongozwa na Askofu mkuu Jude Thaddeus Okolo, Balozi wa Vatican nchini Chad na Bwana
Moussa Mahamat Dabo, Katibu mkuu, Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano na
utengamano wa Afrika amewakilisha serikali ya Chad.
Mkataba huu umegawanyika
katika ibara 18 na utaanza kufanya kazi pale tu pande hizi mbili zitakaporidhia. Vyeti
vinavyotolewa na taasisi za elimu nchini Chad vitaweza kutambulika na Serikali na
kwamba, Kanisa na Serikali vinapenda kushirikiana kwa dhati kwa ajili ya kulinda na
kutetea utu na heshima ya binadamu sanjari na ujenzi wa Jamii inayosimikwa katika
misingi ya haki na amani.