2013-11-07 15:25:40

Heri za Mlimani kuongoza Maadhimisho ya Siku za Vijana Duniani 2014- 2016


Baba Mtakatifu Francisko amechagua tema zitakazoongoza Maadhimisho ya Siku ya za Vijana Duniani kwa kipindi cha Miaka mitatu, kama sehemu ya maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani itakayofanyika mjini Cracovia, Poland, kunako Mwaka 2016. Mada zilizochaguliwa na Baba Mtakatifu ni kutoka katika Heri za Mlimani, ambazo kimsingi ni Muhtasari wa Mafundisho makuu ya Kristo.

Siku ya 29 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2014 itaongozwa na kauli mbiu: "Heri maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Mt. 5:3.

Siku ya 30 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2015 itaongozwa na kauli mbiu "Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

Siku ya 31 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itakayofanyika Jimbo kuu la Cracovia, Poland, itasindikizwa na mada "Heri wenye rehema maana hao watapata rehema." Mt. 5:7.

Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na bahari ya vijana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil, aliwaalika vijana kufanya tafakari ya kina kuhusu heri za Mlimani ili hatimaye waweze kuzimwilisha katika uhalisia wa maisha yao.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba, Heri za Mlimani ni muhtasari wa mafundisho makuu ya Kristo na ni kanuni na mwongozo wa maisha ya kiroho!.







All the contents on this site are copyrighted ©.