2013-11-07 09:52:01

Bagamoyo kumekucha!


Mheshimiwa Padre Galus Marandu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kufunga Mwaka wa Imani kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anabainisha kwamba, hadi sasa maandalizi yamekamilika na wawakilishi kutoka majimbo mbali mbali wameanza safari kuelekea Bagamoyo katika kilele cha Maadhimisho ya Mwaka wa Imani n chini Tanzania hapo tarehe 10 Novemba 2013.

Serikali imeridhia kutoa ulinzi na usalama kwa waamini watakaoshiriki katika Maadhimisho ya Kufunga Mwaka wa Imani yanayoanza rasmi tarehe 8 Novemba kwa njia ya semina za makundi ya Familia ya Mungu nchini Tanzania na kilele chake ni hapo tarehe 10 Novemba 2013.

Baada ya kufunga kwa Mwaka wa Imani, Familia ya Mungu nchini Tanzania itafanya tathmini ya kina kuhusu Mwaka wa Imani na kwamba, Jumatatu tarehe 11 Novemba, 2013, washiriki wataanza kurejea tena majimboni mwao, tayari kuwashirikisha na kumwilisha yale waliyojifunza kutoka Bagamoyo, Mlango wa Imani.







All the contents on this site are copyrighted ©.