Baraza la Makanisa Ulimwengu limechagua wajumbe wa 150 wa Kamati kuu
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, Jumatano tarehe 6 Novemba
2013 wamechagua Kamati kuu ya Baraza inayojumuisha wanachama 150, watakaokuwa na dhamana
la kutoa maamuzi kati ya mikutano mikuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni.
Wawakilishi
hao asilimi 39% ni wanawake, asilimia 61% ni wanaume; vijana wanaunda asilimia 13%,
wawakilishi kutoka katika makundi asilimia ni asilimia 5% na watu wenye ulemavu wanaunda
asilimia 2%. Kati yao Makleri ni asilimia 68% na Waamini walei ni asilimia 32. Majina
haya yamechaguliwa kutoka katika majina yaliyokuwa yamependekezwa na wajumbe 345 wa
Makanisa wanachama.