Mauaji yanayofanywa na Boko Haram ni ukatili dhidi ya binadamu!
Askofu mkuu Ignatius Ayau Kaigama, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria katika
mahojiano maalum na Radio Vatican anabainisha kwamba, mauaji ya kinyama yaliyofanywa
na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram ni kwenda kinyume cha ubinadamu. Watu 35 waliokuwa
kwenye msafara wa harusi walishambuliwa na kuuwawa mwishoni mwa Juma.
Mashambulizi
haya yanaendelea kuongezeka licha ya juhudi za Serikali ya Nigeria kupambana fika
na vitendo vya kigaidi nchini humo. Boko Haram wanafanya mashambulizi ya kushtukiza
kiasi kwamba, inakuwa vigumu kwa vikosi vya ulinzi na usalama kudhibiti vitendo hivi
ambavyo vimeendelea kusababisha majanga kwa wananchi wengi wa Nigeria.
Boko
Haram anasema, Askofu mkuu Kaigama ni tishio kwa usalama, amani, utulivu na maendeleo
ya wananchi wa Nigeria kwa sasa na kwa siku za usoni. Mwanzoni mashambulizi kama haya
yalielekezwa kwa Wakristo, lakini sasa watu wengi wanaendelea kushambuliwa bila huruma.
Serikali inapaswa kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha kwamba, amani na utulivu
vinarejea tena nchini Nigeria kwa kuzingatia utawala wa sheria. Kanisa linaungana
na wote wanaoomboleza kwa kuondokewa na ndugu, jamaa na jirani zao kutokana na vitendo
vya kigaidi. Ni matumaini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria kwamba, iko siku
moja, amani na utulivu vitaweza tena kutawala nchini Nigeria.