2013-11-04 09:07:28

Baba Mtakatifu atembelea na kusali kwenye Makaburi ya watangulizi wake, yaliyoko chini ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro


Katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Marehemu wote, Jumamosi, tarehe 2 Novemba 2013, majira ya jioni, Baba Mtakatifu Francisko alitembelea makaburi ya watangulizi wake waliozikwa chini ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Hija hii ya sala na maisha ya kiroho ilianzia kwenye Kaburi la Mtakatifu Petro, mwamba wa imani Baadaye, Baba Mtakatifu alipita na kusali mbele ya baadhi ya Makaburi kwa kitambo kidogo.

Baba Mtakatifu katika sala yake, amewaweka watangulizi wake waliolazwa kwenye Makaburi yaliyoko chini ya Kanisa kuu la Mtakatifu, wakiwa na tumaini la ufufuko na maisha ya uzima wa milele. Kwa namna ya pekee, amewakumbuka Mapapa ambao walijitosa kimasomaso kwa ajili ya huduma kwa Kanisa la Kiulimwengu, ili waweze kushiriki katika liturujia ya mbinguni.

Hili ndilo tumaini la Mama Kanisa lisilochakaa wala kupitwa na wakati, wakati huu Kanisa linapowaombea watoto wake huruma ili waweze kushirikishwa katika makazo ya Yerusalem ya mbinguni.







All the contents on this site are copyrighted ©.