2013-11-02 10:18:34

Maombi na Baraka za Papa Francisko, kwa Marehemu


Baba Mtakatifu Ijumaa jioni baada ya kuongoza Ibada ya Misa ya Maadhimisho ya Siku ya Watakatifu wote, akiwa katika eneo la Makaburi ya Verano Roma, pia aliwakumbuka marehemu wote na hasa walio fariki jangwani au baharini, hasa wahamiaji na wakimbizi wakiwa katika harakati za kutafua njia mpya za kuboresha maisha yao.

Papa alitoa sala ya utangulizi akisema, Tuombe.
Ee Baba, uliye chanzo pekee cha utakatifu wote ,
Mpendevu katika watakatifu wako wote,
utuwezesha pia sisi kuufikia ukamilifu wa upendo wako
kupitia Ibada ya Ekaristi, inayo dumisha tumaini letu , wakati wa hija yetu hapa duniani, tunapoielekea karamu ya mbinguni. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
R. - Amina
Kisha Papa aliendelea kusema, “ katika muda huu wa kutembelea maeneo ya makaburi, waliko kupumzika ndugu zetu, wake kwa waume, pia unakuwa ni wakati wa kutafakari hali yetu ya kiroho na kufanya upya imani yetu katika Kristo ambaye alikufa , akazikwa na kufufuka tena kwa ajili ya wokovu wetu”.
Papa alikumbusha, hata miili iliyo kufa itatokea katika siku ya mwisho , na wale waliolala katika mapenzi ya Bwana watahuishwa pamoja nae. Aliwasihi wote waliokuwa wamekusayika katika makaburi hayo ya verano, kuinua maombi kwa Baba wa Mbinguni , kwa ajili ya Marehemu na kuomba Baraka zake pia kwa ajili kila mmoja ili kwamba , baada ya kifo , wote waweze pia kukutana mbele ya uso wa Bwana kwa furaha ya uzima wa milele.

Papa aliendelaa kutoa Maombi na Baraka akisema,
“Tubariki , Ee Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
katika huruma yako kubwa, tunafanywa upya kwa
njia ya ufufuo wa Yesu aliyetoka katika wafu, kwa tumaini hai ,
kwa ajii ya kutupatia urithi usio haribiki wala kuoza ;”

“kiliza maombi yetu tunayokutolea wewe Bwana, kwa ajili ya
wapendwa wetu walio tutangulia kuondoka katika dunia hii : fungua mikono yako ya huruma,
na uwapokea wote katika utukufu kanisa Takatifu Yerusalemu.
Na uwafariji wale walio katika maumivu ya kujitenga na wapendwa wao, uwajazea tumaini kwamba Wafu wanaishi ndani yako, na pia hata waliobaki kuzimuni, ipo siku watashiriki katika ushindi wa Pasaka ya Mwana wako.

Papa alikamilisha maombi na baraza akisema , Ninyi ambao katika hija ya Kanisa , mmekuwa ishara ya Mwanga wa Bikira Maria ,kwa njia ya maombezi yake, mdumishe imani , ili kusiwe na kikwazo kinachotaka kubadili njia iendayo kwake, Yeye aliye furaha isiyokuwa na mwisho.

Eee Bwana uwape pumziko la Milele .








All the contents on this site are copyrighted ©.