Wakristu wametakiwa kujua uthabiti wa upendo wao kwa Kristu.
Baba Mtakatifu Francisko , mapema Alhamis hii asubuhi , aliadhimisha Ibada ya Misa,
katika madhabahu ya Mtakatifu Sebastian yaliyoko ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro la Vatican, ambako mwili wa Mwenye Heri Papa Yohane Paulo Yohane II umehifadhiwa.
Katika madhabahu hayo , kila siku ya Alhamis, kikundi cha waamini kutoka Poland hutolea
sala zao katitika Madhabahu haya.Kwa Alhamis hii, mamia ya waamini wakiwemo Mapadre
walihudhuria Ibada . Homilia ya Papa ililenga katika barua ya Mtume Paolo kwa Warumi,
ambamo Mtume Paulo anazungumzia upendo wa Kristu na aya za Injili , ambamo Yesu anaulilia
mji wa Jerusalem alioupenda . Papa Francisko, akitafakari kwa kina masono hayo
anasema , mna sura mbili, zinazoonyesha njia mbalimbali za upendo huu unavyoweza
kupokewa. Kwa upande mmoja , alisema, tunapata uhakika wa upendo wa mtume Paulo
kwa Yesu, kwa maneno yake anaposema, "hakuna mtu anayeweza kunitenga na upendo wa
Kristo ". Mtume Paulo baada ya kuongoka, licha ya kuyaishi mateso ya mwili kwa njia
mbalimbali, ugonjwa na usaliti, upendo wake kwa Kristo ulidumu kuwepo siku zote
za maisha yake, hata saa mwisho ya kifo cha sulubu. Na kwa upande mwingine, Francis
Papa aliendelea , tunaiona huzuni ya Yesu, wakati alipowatazama watu wa Yerusalem
walivyokosa uaminifu katika kuziishi sheria za Mungu. Moyo wa Yesu unaulilia mji
huu, ulioshindwa kuuelewa upendo wa Mungu. upendo huo ambao haukupokelewa.
Papa
Francisko alilinganisha sura hizi mbili, kwanza sura ya Paulo, ambaye anahisi yeye
ni mwenye dhambi , lakini nguvu za imani yake zinatokana na kuupenda upendo wa Mungu,
na sura ya Yerusalemu,ambao watu wake , wanashindwa kuukubali upendo wa Mungu na
wengine wakiupokea kwa hali za mashaka mashaka, wakitawaliwa na ubinafsi wao. Papa
alizitafakari hali hizo na kutoa wito kwa kila Mkristu kujiuliza, je upendo wangu
kwa Yesu ni thabiti kama wa Paulo au ni mashaka mashaka kama ilivyokuwa kwa watu
Jerusalem? Papa alieleza na kutoleo ombi kwa Mwenye Heri Yohane Paulo II, atusaidie
kupata jibu linalo faa katika swali hili.