2013-10-30 09:39:57

Papa kuongoza Ibada ya misa katika makaburi ya Verano Roma.


Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimiso ya Siku ya Watakatifu wote, hapo tarehe Mosi Novemba, atafanya ziara fupi katika jengo lenye makaburi ya tangu zama za kale la Verano Roma, ambako ataongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya maadhimsho ya Siku ya Watakatifu wote.

Ratiba ya mahali hapo inaonyesha kwamba, mwisho wa Ibada hiyo, kipindi cha ukimya wa sala, kwa ajili ya kuwaombea Marehemu wote, na Papa ataobariki makaburi hayo.

Katika Ibada hii Papa atasaidiana na Vika wa Roma, Kardinali Agostino Vallini , pia Askofu Mkuu Fillipo Iannone , Makamu wa Vika wa jimbo la Roma na pia Maaskofu Wasaidzi wa Jimbo la Roma, atakuwepo pia Paroko wa Parokia ya San Lorenzo Nje ya kuta Padre Armando Ambrosi. Papa anafanya ziara hii ikienda sambamba na kumbukumbu ya kupita miaka 20 tangu makaburi hayo yaliipotembelewa na Papa Yoane Paulo II Mosi Novemba 1993.
Makaburi ya Verano ni eneo la Karne nyingi zilizo pita, karne angalau ishirini , kama ilivyoshuhudiwa na kuwepo necropolis Kirumi: huko kuna Makatakombe yanayojulikana kwa jina Santa Ciriaca, yaliyo jengwa wakati wa madhulumu halisi ya utawala wa kirumi dhidi ya Wakristu wa mwanzo.
Ujenzi wa makaburi uliendelea hata baada ya Roma kuendelea kukua hadi kuwa mji Mkuu katika miaka ya (1870-1871) na kulichanganya na viwanja muhimu kama vile ,Mancini Villa liliko kwenye eneo la Pincetto . Lango kuu la kuingia katika eneo hili, lina matao matatu ya kuvutia, pia kuna sanamu nne kubwa zinazo wakilisha tafakari , Tumaini, Huduma na Ukimya. Nyuma ya matao hayo kuna ukumbi mkubwa ambao ni , kazi ya Vespignani ,iliyokamilika mwaka mwaka 1880 .








All the contents on this site are copyrighted ©.