2013-10-30 14:04:42

Askofu Michael Adgum ateuliwa kuongoza Jimbo Katoliki la El Obeid, Sudan


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Oktoba 2013, amekubali ombi la Askofu Macram Max Gassis wa Jimbo Katoliki El Obeid, Sudan la kung'atuka kutoka madarakani kadiri ya sheria za Kanisa 401ยง 1. Wakati huo huo Baba Mtakatifu amemteua Askofu msaidizi Michael Didi Adgum kuwa Askofu mpya wa Jimbo la El Obeid. Kabla ya uteuzi wake, Askofu Adgum alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo hilo hilo la El Obeid.







All the contents on this site are copyrighted ©.