2013-10-28 11:56:44

Balozi mpya wa Japan mjini Vatican awasilisha hati zake za utambulisho!


Baba Mtakatifu Francsiko, Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2013 amepokea hati za utambulisho kutoka wa Bwana Teruaki Nagasaki, Balozi mpya wa Japan mjini Vatican. Bwana Nagasaki alizaliwa tarehe 4 Agosti 1952, ana mke na mtoto. Tangu mwaka 1977 alianza shughuli zake katika masuala ya kidiplomasia na uhusiano wa kimataifa.

Taarifa zinaonesha kwamba, amewahi kutekeleza wajibu huu kama mshauri wa kidiplomasia katika nchi mbali mbali kama vile. Lima, Berna, Helsinki na Barcelona, Hispania. Kuanzia mwezo Agosti 2010 alikuwa ni Balozi wa Japan nchini Guatemala.







All the contents on this site are copyrighted ©.