Vatican na Serikali ya Hungaria watiliana sahihi itifaki ya ushirikiano!
Hivi karibuni, Vatican na Serikali ya Hungaria zilitiliana sahihi mkataba unaofanya
mabadiliko katika itifaki iliyofikiwa hapo tarehe 20 Juni 1997, kuhusu ruzuku ya Serikali
kwa huduma za kijamii zinazotolewa na Mashirika ya Kanisa Katoliki nchini Hungaria
pamoja na baadhi ya masuala yanayohusiana na urithi wa kitamaduni.
Askofu
mkuu Alberto Bottari, Balozi wa Vatican nchini Hungaria aliongoza ujumbe kutoka Vatican
wakati ambapo ujumbe wa Serikali ya Hungaria uliongozwa na Dr. Bence Retvari, Katibu
wa Bunge la Hungaria. Mabadiliko haya yanakwenda sanjari na Katiba ya nchi ya Mwaka
2011.
Katiba imefanya marekebisho kuhusu ruzuku inayotolewa na Serikali kwa
Mashirika ya kidini, elimu ya dini shuleni pamoja na ukarabati wa sanaa za Kanisa
ambazo ni sehemu ya urithi wa wananchi wa Hungaria. Itifaki hii itaanza kutekelezwa
pale ambapo pende zote mbili zitaweza kuridhia vipengele vilivyomo kwenye mkataba
huo!