2013-10-26 07:49:03

Katibu mkuu wa Vatican anawashukuru wote waliomwombea wakati alipokuwa amelazwa hospitalini!


Askofu mkuu Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa amelazwa na hatimaye kufanyiwa upasuaji mjini Padova, kaskazini mwa Italia ameruhusiwa kutoka Hospitali na kwa sasa anapata mapumziko, kabla ya kuanza kazi yake rasmi kama Katibu mkuu wa Vatican.

Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Askofu mkuu Parolin kwa sasa anaendelea vyema na anahitaji mapumziko mafupi kabla ya kuanza utume wake kwa nguvu na ari kuu. Askofu mkuu Parolin anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa uelewa, umakini na uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala wakati wote alipokuwa amelazwa hospitalini.

Anawashukuru wote waliomkubuka kwa sala na sadaka zao. Ni matumaini yake kwamba, ataweza kupona haraka na kuanza utume ambao amekabidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko.







All the contents on this site are copyrighted ©.