2013-10-25 08:39:12

Maadhimisho ya Mwaka wa Imani nchini Angola!


Baraza la Maaskofu Katoliki Angola, Sao Tome na Principe, linafunga Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Jumapili tarehe 27 Oktoba 2013, katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima. Sao Tome, kwa upande wake, itafunga Maadhimisho haya hapo tarehe 24 Novemba 2013.

Baraza la Maaskofu Katoliki Angola linaendelea na mkutano wake wa kawaida wa Mwaka uliofunguliwa hapo tarehe 22 Oktoba na unatarajiwa kufungwa rasmi hapo tarehe 30 Oktoba 2013. Maaskofu kwa sasa wanapanga mikakati ya shughuli za kichungaji kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.







All the contents on this site are copyrighted ©.