2013-10-24 09:25:13

Maandalizi ya Siku ya Wagonjwa Duniani kwa Mwaka 2016


Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Askofu mkuu Zygmunt Zimowski, viongozi waandamizi kutoka Baraza la Kipapa la huduma kwa wafanyakazi wa sekta ya afya pamoja na kikundi cha watu 80 wako Nchi Takatifu katika hija ya maisha ya kiroho. Tayari kikundi hiki kimekwisha tembelea maeneo matakatifu na kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu pamoja na kutembelea baadhi ya Hospitali katika maeneo hayo.

Askofu mkuu Zimowski na ujumbe wake wanatarajia kuhitimisha hija hii ya maisha ya kiroho katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Jumapili tarehe 27 Oktoba 2013. Hija hii ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa Duniani kwa Mwaka 2016 yatakayofanyika mjini Nazareth kwa kuongozwa na kauli mbiu "Kujiaminisha kwa Yesu kama Bikira Maria, "Lolote atakalowaambia, fanyeni".







All the contents on this site are copyrighted ©.