2013-10-23 14:39:38

Papa Francisko kutembelea Ikulu ya Italia!


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Novemba 2013 anatarajiwa kutembelea Ikulu ya Italia kwa mwaliko kutoka kwa Rais Giorgio Napolitano wa Italia, kama sehemu ya mwendelezo wa urafiki kati ya Rais Napolitano na Baba Mtakatifu, alipomtembelea mjini Vatican hapo tarehe 8 Juni 2013.

Hayo yamesemwa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.