2013-10-23 14:45:03

Askofu Franz Peter wa Jimbo Katoliki Limburg asimamishwa uongozi kwa muda


Baba Mtakatifu Francisko baada ya kupewa taarifa rasmi kuhusu hali ya uchumi ya Jimbo Katoliki la Limburg, Ujerumani na baada ya tafakari ya kina, ameamua kumsimamisha katika uongozi wa Jimbo hilo, Askofu Franz Peter Tebartz-Van Elst. Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani kwa kushirikiana na viongozi wa Jimbo hilo wameunda kamati maalum itakayochunguza tuhuma za ubadhirifu wa mali ya Kanisa kutokana na ukarabati wa makao makuu ya Jimbo hilo.

Askofu Franz kwa sasa atakuwa nje ya Jimbo ili kutoa nafasi kwa kamati hii kufanya uchunguzi wa kina na nafasi yake kwa sasa itakaimiwa na Monsinyo Stadtdekan Wolfgan Rosch, makamu Askofu Jimbo Katoliki la Limburg katika kipindi chote cha kutokuwepo kwa Askofu wa Jimbo hilo.







All the contents on this site are copyrighted ©.