Tanzia: Askofu mstaafu Bernardo Felipe Governo amefariki dunia!
Askofu mstaafu Bernardo Felipe Governo wa Jimbo Katoliki Quelimane nchini Msumbiji
amefariki dunia, Jumapili tarehe 20 Oktoba 2013. Marehemu Askofu Governo alizaliwa
tarehe 21 Januari 1939 mjini Macuse, Jimbo Katoliki la Quelimane. Baada ya masomo
na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 4 Oktoba 1969. Tarehe 31 Mei 1976
akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Quelimane. Tarehe 10 Machi 2007 akang'atuka
kutoka madarakani.