2013-10-21 11:11:22

Michezo ni furaha!


Kardinali Gianfranco Ravasi Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni amewapongeza waamini na watu wenye mapenzi mema walioshiriki katika mbio za mita 100 ya imani zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 20 Oktoba 2013 kama sehemu ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani.

Hii inaonesha kwamba, kuna uhusiano wa karibu kati ya imani na michezo na kwamba, michezo inamwezesha mwamini kutolea ushuhuda wa imani yake kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ni mwingi wa huruma na mapendo. Imani ni hazina muhimu inayomwezesha mwamini kufanya majadiliano ya kina na michezo ambayo kila mtu anashiriki kwa kadiri ya kiwango na nafasi yake.

Ni changamoto kwa waamini na watu wenye mapenzi mema kuhakikisha kwamba, michezo inakuwa ni sehemu ya furaha, amani, upendo na mshikamano wa kidugu unaowachangamotisha wanamichezo kuondokana na ubinafsi wao na matendo ambayo ni kinyume cha dhana ya michezo.







All the contents on this site are copyrighted ©.