Balozi Hackett wa Marekani awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 21 Oktoba 2013 amepokea hati za utambulisho
kutoka kwa Bwana Kenneth Francis Hackett, Balozi mpya wa Marekani mjini Vatican. Alizaliwa
tarehe 27 Januari 1947, ameoa na ana watoto wawili. Ni balozi ambaye ana uzoefu na
masuala ya Kanisa kwani tangu mwaka 1972 hadi mwaka 2012 amekuwa ni mfanyakazi wa
Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Marekani.
Kati ya mwaka 1996
hadi mwaka 2004 alikuwa ni Makamu wa Rais Shirikisho la Misaada ya Kanisa Katoliki
Kimataifa, Caritas Internationalis. Kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2010 alikuwa ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Challenge. Na kati ya mwaka 1994 hadi mwaka 2012
alikuwa pia ni mjumbe wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki,
Cor Unum.