Ujumbe wa Papa kwa Mkutano wa Wakatoliki Ufilipino
(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko, kwa njia ya Video , Ijumaa alituma ujumbe
wake kwa washiriki wa Mkutano uliohudhuriwa na wajumbe karibia elfu tano kutoka eneo
la Kusini mwa Asia. Mkutano huu uliandaliwa na Jimbo Katoliki la Manila , na ulikamilika
siku ya Ijumaa 18.10.2013. Mkutano huu wa siku tatu, ulilenga zaidi hoja ya
Uinjilishaji Mpya, na umekamilika na malengo makuu matatu: kujenga uzoefu wao kwa
Mungu katika mazingira ya milenia mpya. Kuimarisha vifungo vya ushirika na umoja
katika eneo la KusIni mwa Asia, Na uwepo wa kishindo cha msukumo mpya wa kuishi
na roho aminifu katika imani na utume .Mkutano huu ulifungwa kwa Ibada ya Misa iliyoongozwa
na Mjumbe wa Papa nchini Ufilipino, Askofu Mkuu Giuseppe Pinto.
Kwa njia ya
video , Papa alisoma ujumbe kwa washiriki wa mkutano huu , akionyesha kufurahia
kwamba, Mkutano juu ya Uinjilishaji Mpya, ni sadaka sitahili katika maadhimisho ya
Mwaka wa Imani. Kwa hili, aliwashukuru wote, Maaskofu , mapadre, watawa wa kiume
na wanawake, seminaristi, na walei, kwa ushiriki. Na kwa kutoka sehemumbalimbali za
Ufilipino na Asia , hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao,
na hivyo Kanisa la Kristo ni hai!
Papa alionyesha tumaini lake kwamba kupitia
a mkutano huo , wameweza kupata uzoefu mpya wa uwepo wa upendo wa Yesu katika maisha
yao, na hivyo watalipenda Kanisa zaisi na zaidi wakiushirikisha upendo ya Kiinjili
kwa watu wote kwa unyenyekevu na furaha. Papa amewasihi wasichoke kuipeleka huruma
ya Baba wa Mbinguni kwa maskini , wagonjwa, walio telekezwa, vijana na familia.
Na waweze kufanikisha kumtangaza Kristu katika ulimwengu wa siasa , biashara, sanaa,
sayansi, teknolojia na vyombo vya habari vya kijamii.
Papa aliomba Roho Mtakatifu
afanye upya viumbe wa Mungu ili waweze kutoa matunda ya haki na amani katika Philippines
na katika bara la Asia kwa ujumla. Papa alisema wote ndani ya moyo wake. Na Aliwaomba
pia wamkumbuke katika sala , nae akaahadi kuwaombea, na hasa maombezi ya mama yetu
Bikira Maria , Nyota ya Uinjilishaji Mpya .