2013-10-18 15:31:25

Sr Eugenia Bonnini apokea tuzo ya Umoja wa Ulaya


(Vatican Radio) Sista Eugenia Bonetti wa Shirika la Wakosolata, Muitaliani , mtawa wa kwanza kuonyesha kujali kwa makini zaidi dhidi ya biashara haramu ya ukahaba, mwanzilishi wa juhudi za kupambana na biashara hiyo haramu, ni miongoni mwa waliopokea Tuzo ya Raia wa Ulaya ya mwaka 2013.

Tuzo ya kila mwaka iliyozinduliwa na Bunge la Ulaya mwaka 2008 kama kutambua mafanikio ya kipekee kwa raia mmoja mmoja au vikundi vya watu ambao wameweza kushirikiana vyema na Umoja wa Ulaya, katika kukuza maelewano zaidi kati ya wananchi wa Ulaya na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Pia tuzo hutolewa kwa ajili ya utendaji wa shughuli za siku hadi siku, zinazo lennga kuonyesha maadili yanazingatiwa katika mkataba wa EU katika haki za msingi za binadamu .

Sr Eugenia , ambaye ni mwenyekiti wa Juhudi zinazoitwa "Utumwa hakuna tena," “Slaves No More ' shirika lisilo la kiserikali na mratibu wa Watawa Mama Wakuu wa Italia, katika kupambana na biashara haramu ya ukahaba kwa Wanawake na Watoto , alianzisha mapambano haya dhidi ya aina hii ya utumwa mambo leo, miongo miwili iliyopita.
Akizungumza na Philippa Hitchen, katika mahojiano, Sista Bonneti alisema, Juhudi hizi alizianzisha mwaka 1993, wakati alipomtazama mwamwake wa Kiafrika, akiwa amesimama pembezoni mwa barabara, akisubiri wateja, kama ilivyo kawaida kwa mitaa mingi ya miji mikubwa ya Italy na ulaya.
Sr Eugenia, ambaye kwa karibia miaka 30 alifanya utume wake barani Afrika, kama mmisionari, alishtushwa kuona jinsi wasichana wengi vijana, hasa Wanigeria lakini pia kutoka mataifa mengine ya Afrika , wakifanya ukahaba kama iivyokuwa kuwa pia katika mji wa nyumbani kwake wa Turin. . Na maisha yake Sista Eugenia yalibadilishwa na mmoja wa wasichana hao , Maria, aliyefika katika kituo cha Caritas ambako alikuwa akifanya kazi, ambaye alimfuata baada ya Ibada ya Misa na kumpa changamoto katika maisha yake ya kitawa, hasa kuhusu huduma ya kidini na utume wake wote. Kwa kifupi , anasema, Maria akawa Katekisti yake, iliyomsaidia kuelewa njia tata wanayo ipitia wengi wanawake na wasichana wanao simama kando ya barabara, kumbe hununuliwa na kuuzwa , kupigwa na kubakwa na kuishia kufanya kazi ukahaba mitaa katika nchi zinazojiita zimesitaarabika.

Katika maeelezo yake alitaja kwamba, leo hii kuna waathirika milioni 27, katika biashara hii haramu ngazi ya kimataifa, ambayo inakadiriwa kuhusisha kiasi cha dola bilioni 32 kila mwaka.
Kwa miongo miwili iliyopita, Sr Eugenia amekuwa mstari wa mbele kufanikisha juhudi za Kanisa Katoliki hapa nchini Italia, kupambana na biashara hii inayofanyika dhidi ya ubinadamu, kuvunja minyororo ya mfumo huu wa utumwa wa kisasa, na kuwasaidia wanawake wanaosafirishwa, kurejesha hisia ya matumaini na heshima katika maisha yao yaliyopoteza matumaini .








All the contents on this site are copyrighted ©.