Rais Paul Biya akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 18 Oktoba 2013 amekutana na kuzungumza na
Rais Paul Biya, Rais wa Cameroon ambaye pia alikutana na Askofu mkuu Dominique Mamberti,
katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.
Viongozi
hawa wawili katika mazungumzo yao wamepongeza uhusiano mzuri uliojengeka kati ya Vatican
na Cameroon na kwamba, kwa pamoja wameonesha matumaini katika mchakato unaotaka kuhitimisha
mkataba kati ya Vatican na Cameroon kuhusu nafasi ya Kanisa Katoliki kisheria nchini
Cameroon. Makubaliano haya yanatarajiwa kutiwa sahihi katika kipindi cha siku chache
zijazo!
Viongozi hao wamelipongeza Kanisa Katoliki nchini Cameroon kutokana
na mchango wake kwa wananchi katika medani mbali mbali za maisha, hususan katika sekta
ya elimu, afya; haki, amani na upatanisho.
Baba Mtakatifu Francisko na Rais
Paul Biya wamegusia pia changamoto ambazo Bara la Afrika linaendelea kukabiliana nazo
sanjari na mchango wa Cameroon katika kuimarisha mchakato wa amani na uptanisho Barani
Afrika.