2013-10-18 09:39:02

Papa kufanya mafungo ya Kwaresma nje ya Vatican


Baba Mtakatifu Francisko katika Maandalizi ya Siku kuu ya Pasaka kwa Mwaka 2014, ataungana na wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya Mafungo ya Kipindi cha Kwaresima, ambayo kwa Mwaka 2014 yatafanyika kuanzia tarehe 9 Machi hadi tarehe 14 Machi 2014 mjini Albano, nje kidogo ya mji wa Roma. Mafungo haya yataongozwa na Monsinyo Angelo De Donatis kutoka Jimbo kuu la Roma.

Habari hizi zimethibitishwa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican na kwamba, lengo na kufanya mafungo haya ya kiroho nje ya mji wa Vatican ni kuwawezesha wahusika wakuu kupata nafasi ya ukimya na utulivu ili waweze kupata nafasi ya kusali, kutafakari na kufunga; mambo msingi katika hija ya maisha ya kiroho kwa waamini.







All the contents on this site are copyrighted ©.