Siku ya Chakula Duniani 2013:Papa akemea kashfa ya njaa na utandawazi wa kutojali
matokeo yake mabaya.
Katika kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani, Oktoba 16, 2013, Ujumbe wa Papa Francisko
umelaumu mwendelezo wa kashfa ya njaa na utapiamlo katika dunia ya leo na kile alichokiita
utandawazi wa kutojali kama matokeo yake mabaya.
Hotuba ya Papa Francisko
ilitolewa na Monsignor Luigi Travaglino , wakati wa sherehe za Siku ya Chakula Duniani,
zilizo fanyika Makao Makuu Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, yaliyoko
hapa Roma. Katika ujumbe huo, Papa amekosoa kile alichokiita " kukua kwa mwelekeo
wa binadamu kutojali hali za wengine ambako huongoza katika tabia ya kubaguana,iwe
kati ya mtu na mtu , kama taasisi au hata katika ngazi ya nchi kwa nchi. Na hasa
katika namna za kujali tatizo la uhaba wa chakula, na njaa kali kwa baadhi ya watu
, kama vile ni janga lisilo weza kuepukika.
Papa ametoa wito kwa jumuiya
ya kimataifa, kuvunja ubinafsi na utumwa wa watu wchache kutaka faida kubwa kwa
gharama zote, si tu katika mahusiano ya binadamu lakini pia katika mienendo ya kimataifa
ya kiuchumi na kifedha. Ili kuishinda njaa , amesema, watu wenyewe wanahitajika kujielimisha
upya, juu ya thamani na maana ya mshikamano, neno linaloonekana kukera na kuondolewa
katika lugha ya wenye navyo.
Papa amekosoa ubinafsi huo, akitazamisha
katika ukweli kwamba, karibia moja ya tatu ya chakula chote kinacho zalishwa duniani
huishia katika mapipa ya taka.Na hivyo anasema, kuna haja ya kurekebisha mitindo ya
maisha, ikiwa ni pamoja na mazoea ya kula. Uharibifu huu wa chakula , anaoonekana
ni matokeo ya utamaduni wa kutupilia mbali, ambao kwa mara nyingi hutokana na roho
ya ubinafisi na ubabe wa wanaume na wanawake, kuabudu miungu ya faida na ulaji.
Papa
ameutaja udhaifu huo kuwa ni, ishara ya kusikitisha , zinazo onyesha utandawazi wa
kutojali wengine ambao, taratibu hutufanya kuyazoea mateso ya wengine na kuona kama
ni maisha ya kawaida kwao.
Alihitimisha ujumbe wake kwa wito wa elimu katika
mshikamano na maisha kwa ajili ya kupata ushindi dhidi ya utamaduni wa tupatupa au
ukimwanga wenye kudharirisha hadhi ya ubinadamu na heshima yake. Ametaka ubinadamu
na utu wake uwe kiini cha kuthaminiwa sana katika hatua zote za maisha, ustawi na
maendeleo ya kila mtu. .