2013-10-16 15:33:55

Papa Francisko , aagana Kardinali Tarcisio Bertone, kama Katibu


(Vatican Radio) Jumanne licha ya kutokuwepo Katibu Mpya wa Jimbo la Papa , Askofu Mkuu Pietro Parolin, Papa Francisko, alikutana na Kardinali Tarcisio Bertone, SBC, Katibu wa Vatican, aliyemaliza kipindi chake cha kuwa “Camerlengo” wa Kanisa Katoliki , na Katibu wa Jimbo la Papa kwa ujumla, kwa nia ya kuagana katika utume huo.

Papa Francisko, katika maelezo yake ya kuagana, alisema, ndugu yangu, umefika wakati wa kutoa kifimbo cha huduma ya Katibu kwa Jimbo la Papa , kwa mtu mwingine. Na hivyo ninapenda kuungana nawe kiroho, kumshukuru Mungu kwa ajili ya mema mengi aliyokujalia katika kufanikisha utume huu muhimu na nyeti na kama changamoto. Papa Francisko alimwambia na kumweka katika maombezi ya Mtakatifu Theresa wa Yesu, ambaye Mama Kanisa alifanya kumbukumbu yake kilitulujia siku ya Jumanne, akimwalika pia aendelea kuyakaza macho yake kwa Mungu, asiyewatupa waja wake, kama mtakatifu huyu Mkuu wa avila alivyosema, basi kusiwe na chochote cha kuwatisha ninyi; wenye kumcha Mungu, na msikose majaliwa yake.

Papa Francisko, kwa niaba yake na kwa niaba ya Papa Mstaafu Benedikto XVI, alimshukuru kwa dhati Kardinali Bertone, kwa bidii na utumishi wake mzuri alioonyesha katika kulitumikia Kanisa katika miaka hii zaidi ya saba, baada ya kuitwa kutoka Genoa , ambapo alikuwa Askofu Mkuu , Na kurudi Roma, kuchukua nafasi ya Katibu wa Jimbo la Papa tangu 15 Septemba 2006, na hivyo pia kuwa Camerlengo wa Kanisa Katoliki la Ulimwengu. Papa amekitaja kipindi hiki cha miaka saba kuwa ilikuwa ya kazi nyingi na pengine ngumu, lakini aliweza kukiishi kwa ukarimu mkubwa, katika roho ya huduma. Na pia katika kipindi kifupi alichofanyakazi pamoja nae , ameweza kufaidika na mengi siku hadi siku, kwa utaalam na ushirikiano wake.

Na mwisho Papa Francisko , alipenda kutoa shukurani zake za Kipekee kwa uaminifu wa roho yake, roho ya Don Bosco na roho ya Wasalesian , katika uwezo wa kuhifadhi na kushuhudia Injili ya Kristu , licha ya uwepo wa kazi nyingi, kwa ajili ya mshikamano na Khalifa wa Petro. Na kwa upendo unaoonyesha tabia ya Mtakatifu Don John Bosco, ya majitoleo ya kiroho na kimwili bila ya kujibakiza, katika kazi yake ya kuongoza, mahusiano ya kimataifa ya Jimbo Takatifu, utendaji muhimu sana katika zoezi zima la huduma ya Askofu wa Roma duniani. Na wakati huo huo, bila ya kuepa jitihada zozote zilizo lenga kufakisha mafundisho ya Papa na baraka za Kitume kila mahali: kwa nchi zote , majimbo, mihadhara, vyuo vikuu, taasisi, mashirika, vyama na jumuiya za kitume.

Papa Francisko alihitimisha maelezo yake kwa kumwomba Mama Yetu Bikira Maria, Msaada wa Wakristo, daima awe karibu na Kardinali Tarcisio Bertone, katika huduma yake ya thamani. Kwa maombezi yake ya kimama,Bwana amjalie tuzo mbinguni na neema kwa moyo wake mpendevu. Na pia Baraka zake za Kitume, zimwezesha kupata amani na furaha ya kiroho, yeye mwenyewe Kardinali Bertone na pia kwa wafanyakazi wenzake na wapendwa wake wote.








All the contents on this site are copyrighted ©.