2013-10-16 15:55:52

Hotuba ya Kardinali Tarcisio Bertone kwa Papa wakati akiaga rasmi cheo cha Katibu wa Jimbo la Papa


Kardinali Tarcisio Bertone, katika kuhitimisha utume wa kuwa Katibu wa Jimbo la Papa , Oktoba 15, 2013, aliagana na Papa Francisko, kwa maneno yaliyotoka ndani ya roho ya Wasalesiano , na pia kwa Mtakatifu Ignatius wa Loyola, na pia kwa moyo wa Don Bosco. Kardinali Bertone aliagana na Papa wakiwa katika Chumba cha Mkitaba ya Papa, mjini Vatican , ambamo Kardinali alitoa shukurani zake dhati wa Papa Francisko, akisema, asante sana.
Na aliainisha kuhitimisha kwa majukumu yake kama Katibu wa Jimbo la Papa sanjari na Hija Fatima, katika maadhimisho ya tukio la Mwisho la Bikira Maria kuwatokea watoto wa Fatima , na pia kwa ajili ya kutimia miaka 60 tangu kujengwa kwa Basilika la Rozari Takatifu Fatima, kama alivyosema muumini mmoja, kwenda kwake katika madhabahu hayo, kuhitimisha kazi yake ya kuwa Katibu, ilikuwa sawa na kukabidhi ufunguo wa dhahabu.

Kardinali Bertone, katika maelezo yake amekiri, ni ngumu kwake kutoa muhtasari wa kina juu ya miaka saba ya utumishi wake kama Katibu kwa Papa Benedict XVI na, kwa kipindi kifupi cha Papa Francisko. Lakini ametaja mambomuhimu aliyoyaweka moyoni mwake kama kumbukumbu, ni umuhimu wa kufanya kazi kwa ukaribu na kila mtu, katika ufanikishaji wa kazi pamoja , licha ya kuwa na majukumu tofauti na majitoleo binafsi ambayo wakati mwingine ni sadaka. Kardinali ametoa shukurani zake kwa wote.

Kardinali alieleza pia kilichomvutia kwa Papa Benedict XVI, ni mtazamo na uelewa wake wa juu Kanisa kama ni ushirika katika kina kirefu, na pia uwezo wake katika kuzungumza na ulimwengu na kugusa mioyo na akili ya watu wengi, kupitia mafundisho yake yenye uwazi na kina cha fikira. Na kwamba Papa Benedict XVI alikuwa ni mtengenezaji wa majiundo ya dhamiri na Makleri. Utawala wake kama Papa , uiliweka nguvu zaidi katika utume wa kichungaji, kwa kuwa na matukio kadhaa muhimu kama kuitisha Mwaka Mtakatifu Paulo, Mwaka kwa ajili ya Mapadre, na Mwaka wa imani.
Karidinali Bertone pia amedokeza vipindi vigumu vilivyo umiza moyo wa Papa Benedikto XV1, kwa ndani kwamba ni uchungu kwa maovu yanayochafua sura nzuri ya Kanisa. Na kwa ajili ya kutunza utakatifu wa Kanisa, aliweka sheria mpya, katika kukabiliana na hali ya aibu ya viongozi wabovu wa kanisa, wenye kuchafua uso wa kanisa kama kasha ya madhulumu ya kijinsia kwa watoto. Pia bila ya kusahau uzinduzi wa sheria mpya ya kiuchumi na kiutawala kwa jimbo la Papa .
Na kwamba , Bwana alimwongoza katika uvuvio wa kiroho, baada ya kutafakari na maombi ya makali ya kina, alichukua uamuzi wa kujiondoa katika huduma utume wa Petro, kama alivyoongozwa na Roho wa Yesu.
Kardinali Bertone pia alitaja kwa muhtasari juu ya Papa Francesko, akisema, juhudi anazozifanya si kwamba anafanya mapinduzi, lakini anaendeleza mawazo ya Papa Benedilto XVI, kwa utajiri wa utofauti wa lugha na uzoefu wa maisha, kulingana na asili yetu na njia yetu, kama yeye mwenyewe Papa Francisko anavyosema , tuko pamoja katika utajiri wa utofauti wetu. Na maelewano ni jambo la msingi na njema. Kusikiliza , huruma, rehema, na imani maajabu ya ukweli kwamba, ambao Papa Francisko yeye mwenyewe binafsi anauzoefu nao, kama anavyoendelea kueleza katika mazungumzo yake.

Na amemshukuru Papa Francisko kwa wema wake! Na ameomba kwa Maria, awe msaada daima kwake Yeye Papa Francisko na Katibu mpya wa Jimbo, Mheshimiwa Askofu Mkuu Monsignor Pietro Parolin , ili kanisa zima la Ulimwengu lipate kufungua mafundo yote yanayozuia bado Kanisa la Kristo, kuwa katika moyo wa upeo wa macho ya dunia zima, ambalo ni ombi la kina kwetu sote. Asante, Baba Mtakatifu!








All the contents on this site are copyrighted ©.