Papa Francescisko amemteua Kardinali Peter Erdo, Askofu Mkuu wa Esztergom-Budapest,
kuwa Msimamizi Mkuu wa Sinodi Maalum ya Maaskofu, itakayofayika 5-19 Oktoba 2014,
juu ya "Changamoto za Familia katika mtazamo wa Uinjilishaji mpya". Pia kwa ajili
hiyo, Papa amemteua kuwa Katibu Mkuu wa sinodi hiyo, Askofu Mkuu wa Bruno Forte,
wa Jimbo Kuu la Chieti-Vasto. Jimbo la Uvira lapata Askofu mpya Baba
Mtakatifu Francisko , Jumanne 15 Octoba 2013, amemteua kuwa Askofu wa Jimbo la Uvira
Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, Monsiyori Sèbastien Muyengo Mulombe. Hadi kuteuliwa
kwake alikuwa ni AskofuMsaidizi wa Jimbo Kuu la Kinshasa. Kapanda Cheo Padre
Fernando Vèrgez Alzaga , kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa utawala katika nchi ya
Vatican, Baba Mtakatifu amempandisha cheo na kuwa Askofu wa Jina wa Villamagna di
Proconsolare.