2013-10-15 10:24:03

Baraza la Mawaziri Malawi lavunjwa kwa rushwa na ufisadi!


Rais Joyce Banda wa Malawi, mwishoni mwa juma amevunja Baraza la Mawaziri kwa tuhuma za kujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma pamoja na ufisadi. Uamuzi wa Rais Banda unatokana na manung’uniko ya wananchi kwa Mawaziri 25 kwamba walikuwa wanajihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, hali iliyopelekea wafadhili wakuu wa Malawi kutishia kusitisha misaada yake nchini Malawi, ikiwa kama Rais Joyce Banda angeshindwa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Mawaziri wake.

Wakati huo huo, Rais Banda ameunda tume maalum ili kuchunguza fedha ya umma na kwamba, masuala ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa kwa sasa yatasimamiwa na Ofisi ya Rais hadi pale mawaziri wapya watakapokuwa wameteuliwa tena.








All the contents on this site are copyrighted ©.