Jinsi nina hamu ya Kanisa kuwa maskani kwa ajili ya maskini!”
Kwa maneno haya aliyoyatamka mara tu baada ya kuchaguliwa kwake kama Baba Mtakatifu,
Jorge Bergoglio aliigusia mada ambayo imeendelea kuwa ndicho kipaumbele cha kwanza
na kiini cha uongozi wake kama Papa. Si kitu cha kushangaza kwamba watu wengi wamesema
kwamba maneno kama haya yanaonyesha kwamba Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakatoliki
kuwa makini na kutolea muda wao katika mchakato wa kupambana na baa la umaskini. Kwa
upande mmoja, haya ni kweli. Hata hivyo ni tafsiri iliyopungukiwa na maana halisi
na ya ndani zaidi ambayo Francis mwenyewe anaiambatanisha na umaskini.
Mtu
yeyote hapaswi kushangaa kwamba Francis anaongea sana juu ya hali ya umaskini, kwani
yeye mwenyewe ni mwenyeji wa Amerika ya Kusini: sehemu ya ulimwengu ambapo mamilioni
ya watu (isipokuwa Chile) wanaishi kwenye umaskini mkuu. Utakuwa umekosa utu usipoguswa
na tofauti za kutisha kati ya Recoleta ambao ni mji mzuri na wa kupendeza wa Buenos
Aires, unao ufanya mji huo kujulikana kama Paris ya Kusini, na hali duni ya maisha
ya vitongoji kama vile Rodrigo Bueno.
Wakristo hawana budi kuguswa na tofauti
kama hizi. Lakini ili tuyaelewa maneno ya Francis juu ya umaskini lazima tuelewe kwamba
Baba Mtakatifu ni Mkatoliki haswa. Yeye sio mwanafalsafa au mchumi mtendaji (practical
materialist). Kwa hivyo, ung’amuzi wa Papa Francisko juu ya maskini na umaskini unapita
ule uelewa wa kawaida wa kijamii kuhusiana na maswala haya.
Katika cha kusisimua
cha maswali na majibu kwenye vigilia ya Pentekoste ya mwaka huu, pamoja na washiriki
wa vyama vipya katika Kanisa (new movements) ambavyo vimechangia sana kuleta uhai
ndani ya Kanisa tangu Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, Baba Mtakatifu aliyasema haya
kuhusu Ukristo na Umaskini.
Kwetu Wakristo umaskini sio swala la kijamii, kifalsafa
au kitamaduni. La hasha, bali ni swala la kiteologia. Ningesema pengine swala la kwanza,
kwani Mungu Mwana alijishusha, akajifanya maskini ili kuweza kuambatana nasi kwenye
njia yetu. Na huu ndio umaskini wetu: umaskini wa mwili wa Kristo, umaskini ambao
mwana wa Mungu alituletea kwa kujifanya mtu kwake. Kanisa maskini kwa ajili ya maskini
linaanza kwa kuuelekea mwili wa Kristo. Tukiuelekea mwili wa Kristo, tutaanza kuelewa
kitu, kumbe tutaelewa maana hasa ya umaskini huu, umaskini wa Bwana.
Kwa neno
moja, hili linagusia unyenyekevu. Kama Myesuiti mwingine, Philip Caraman, alivyoandika
wakati mmoja, unyenyekevu ni fadhila “ambayo kwayo tunajipima kisawasawa mbele ya
Mungu, tukitilia maanani yote yale ambayo Mungu ametupa, ametufanyia, na anayotarajia
kutoka kwetu.”
Uelewa mwingine unatokana na kukumbuka kwamba neno la Kigiriki
lililotumiwa kwenye Injili ya Mathayo(5:3) kuelezea “umaskini wa kiroho” (πτωχός)
lina maana ya kushushwa hadi kuwa mwombaji. Kwa sababu hiyo, maskini wa kiroho ni
wale kati yetu – maskini, tajiri, wenye kipato cha kati – wenye kuzifahamu dhambi
zetu na kumwomba Kristo atuokoe.
Hiki ndicho kiini cha nini hasa maana ya Kanisa
Maskini. Kanisa nyenyekevu sio Kanisa lenye uoga, lenye waumini wenye kunyong’onyea
kwenye mambo ya imani; bali ni Kanisa ambalo linawajumuisha watu ambao, kwa uhuru
kabisa, wanajitoa kidete kwa Kristo aliye peke yake mwenye uwezo wa kutuokoa.
Hayo
pia yanajiri kwenye tafakari juu ya maisha ya Mtakatifu Francisko wa Assisi. Hapa
ni vizuri kuonesha pengo lililopo kati ya riwaya zisimuliwazo juu ya Francisko, na
ukweli hasa juu ya mtu huyu.
Kwa mfano, katika wake wa hivi karibuni juu ya
Francisko, Mdominikani Augustine Thompson, anaonyesha kwamba mazungumzo yaliyosifika
sana kati ya Francisko na Sultan al-Kamil wa Misri hayakuchangiwa na hisia zozote
au harakati dhidi ya vita. Kwake Francisko, lengo la tendo hili lilikuwa kumbadilisha
Sultan huyo kuwa Mkristo!
Pia Thompson anaonyesha ukosefu wa subira wa Francisko
juu ya ulegevu kwenye maswala ya Kiliturjia, ukosefu wake wa kujihusisha na aina yoyote
ile ya programu za kisheria au mageuzi ya kijamii, uwezo wake wa kubainisha kati ya
umaskini hohe hahe na ule wa kawaida, na pia hakushikilia itikadi na fikira zilizojiri
kwa wakati wake kuhusiana na Mungu na Mazingira au Pantheism kwa lugha ya Kimombo;
na kwamba kitu asichokuwa akitazamia kabisa Francisko ni kwa shirika lake kugeuka
kuwa kikundi cha wafanyakazi wa kijamii au social workers. Mtakatifu Francisko, anaendelea
kusema Thompson, alikuwa mkakamavu wa imani, na kwamba Francisko alikuwa mtii kwa
Mungu na Kanisa, akimaanisha uongozi wake mathubuti.” Katika wosia wake wa mwisho,
Fransisko hata alisisitiza kwamba waasi au wakiukaji wa sheria ambao wangejitokeza
kwenye shirika lake watolewe kwa serikali ili iwashughulikie kulingana na sheria za
nchi.
Kutokana na yote haya, inakuwa vigumu kumwona Francisko kama mpinzani,
au mtetezi na mwanaharakati wa namna yoyote ile. Hata Wakatoliki wengine hushangaa
wanapogundua kwamba uelewa wa Francisko juu ya umaskini haukuwa unapinga tofauti za
kijamii juu ya kipato au kuwaonea wivu matajiri. Thompson anaonyesha kuwa Mtakatifu
huyu aliandika kidogo sana juu ya umaskini, na wakati alipoandika, haikuwa na uhusiano
na “kujibandua kabisa na mali, maisha ya kawaida, au kuishi tu kwa siku hiyo.” Bali
ilikuwa hasa kuhusiana na ukweli kuhusu Nafsi ya Pili ya Utatu Mtakatifu aliyejishusha
na kuchukua hali ya kibinadamu katika umwilisho na kujitoa sadaka kwa ajili ya binadamu
wote kwa kufa Msalabani.
Kwa hiyo, kulingana na Thompson, mtazamo wa Mtakatifu
Francisko kuhusu umaskini ulikuwa hasa ni “kujikana mwenyewe, kutoa huduma kwa ajili
ya Mungu na kuyatii Maandiko Matakatifu yanayohubiriwa na Kanisa la Kristo. Kwa maana
hiyo, mawazo ya Francisko kuhusiana na umaskini, kama alivyoandika Thompston , siyo
ya “kisiasa.” Ila ni kuhusu kuufikia utajiri wa kiroho unaotokana na kumkumbatia hasa
Kristo.
Je, hili linatuambia nini kuhusiana na jinsi wakatoliki wanapaswa
kuwaza juu ya umaskini? Kwanza kabisa, ukereketwa wa kisiasa usiwe ndicho kitu
cha kwanza kufikiria tunapoongea juu ya kukomesha umaskini. Sio bure kwamba Baba Mtakatifu
Francisko kwenye mahubiri yake ya vigilia ya siku ya Pentecost alisisitiza kwamba
“Kanisa sio mfumo wa kisiasa, au chama fulani, na kwamba kama Kanisa... sisi si Shirika
lisilo la Kiserikali (NGO), na kwamba, Kanisa linapokuwa NGO, linapoteza chumvi na
ladha yake, na hivyo linabaki kama chama tu, bila uhai.”
Ni kweli kwamba
wa Baba Mtakatifu Francisko kwa serikali kuzingatia majukumu yao hasa kuhusiana na
maswala ya uchumi wa kimataifa, unatokana na uhakika wake kwamba kuna jukumu la kisiasa
katika kukabiliana na umaskini. Ila maandishi yake kabla ya kuchaguliwa kuwa Papa
yanabainisha kwamba Francisko analiona hili kwani hapo 2011 (wakati uchumi wa Argentina
ulipoanguka), Bergolio aliandika kwenye jarida la , kwamba “kuna waagentina wanaokumbwa
na umaskini na kusukumwa pembezoni mwa jamii, ambao ni lazima tuwachukulie kama wadau
na wahusika katika kuchonga hatima ya maisha yao wenyewe, na sio tu kama wafaidi wa
misaada inayotolewa na serikali na mashirika ya kijamii”.
Lakini zaidi ya yote
Francisko anawataka wakatoliki kuonyesha mwanga wa kikristo katika kukabiliana na
swala la umaskini. Katika hotuba yake ya vigilia ya Pentekoste, alisisitiza kwamba
lengo letu la kwanza lisiwe nguvu tendaji na kufanikiwa. “Ni kitu kimoja kumhubiri
Yesu,” Francisko aliwaambia wasikilizaji wake, “na kitu kingine kufanikiwa.”
Haimaanishi
kwamba wakristo hawana wajibu wa kufikiri na hata kujadiliana jinsi ya kuukomesha
au kuupunguza umaskini. Ndivyo inavyodai haki. Francisko anataka kutuonyesha kwamba
ikiwa tutashughulikia tu “mafanikio kwa mtazamo wa kidunia”, kuna hatari ya kuusahau
upendo wa Kikristo.
Katika kuendeleza mjadala wake, Papa Francisko aliwauliza
maswali mawili wale waliokuwa wakimsikiliza: “Niambieni, unapomsaidia mtu aneyeomba
njiani, unamwangalia machoni baba au mama huyo?. . . Na unapomsaidia, unamshika mkono
unayemsaidia au unamrushia tu vishilingi?” Mambo matatu—kama asemavyo Francisko!—yanajitokeza
hapa. Moja ikiwa ni: mara ngapi sote tumeanguka mtihani huu?
Pili ni Mwenyeheri
Theresa of Calcutta. Hakuwa na mawazo ya kufanikiwa alipoamua kuwahudumia walio hoi
zaidi miongoni mwa watu wa dunia. Katika maisha yake, alikaripiwa kwa kutokujihusisha
zaidi kisiasa kuhusu baa la umaskini. Ila kazi yake haikuwa ya kisiasa. Ilikuwa juu
ya kitu ambacho ni kikuu kuliko siasa: kuuleta upendo wa Kristo kwa wale ambao Kristo
mwenyewe alituambia tutauona uso wake ndani mwao.
Na tatu ni kile ambacho
Papa mstaafu Benedicto XVI alisisitizia sana kwenye waraka wake wa kwanza wa kipapa,
, Mungu ni Upendo. Ijapokuwa waraka huu ulisisitiza sana maswala ya haki, Benedict
wa kumi na sita alikazia kwamba kuna kitu ambacho kila mtu anayekumbwa na mateso anakihitaji
zaidi: “upendo wa kipekee na kuthaminiwa.”
Kwao Baba Mtakatifu Francisko, mtangulizi
wake (Benedikto wa kumi na sita), na Mwenye heri Mama Theresa (Wa Calkutta), jibu
letu kuhusiana na umaskini lazima liwe, juu ya yote, kuonyesha haswa huruma, ambayo
ndiyo kiini cha Injili. Pamoja na mambo mengine, hii inasaidia kusahihisha ule mwelekeo
wa kibinadamu kwamba haki tu inatosha. Mungu angekuwa ni Haki tu, bila Upendo asingeweza
kushuka na kuingia kwenye historia ya wanadamu kwa umbo la Yesu Kristo ili kutuokoa
kutokana na sisi wenyewe. Tulikuwa hatumdai Mungu chochote. Kwa maana hiyo, basi,
uelewa wa Kikatoliki kuhusu umaskini unatukumbusha kwamba ni Huruma ya Kimungu, na
sio haki, ambayo inatuokoa.
Kwa maneno haya aliyoyatamka mara tu baada ya kuchaguliwa
kwake kama Baba Mtakatifu, Jorge Bergoglio aliigusia mada ambayo imeendelea kuwa ndicho
kipaumbele cha kwanza na kiini cha uongozi wake kama Papa. Si kitu cha kushangaza
kwamba watu wengi wamesema kwamba maneno kama haya yanaonyesha kwamba Baba Mtakatifu
Francisko anawataka wakatoliki kuwa makini na kutolea muda wao katika mchakato wa
kupambana na baa la umaskini. Kwa upande mmoja, haya ni kweli. Hata hivyo ni tafsiri
iliyopungukiwa na maana halisi na ya ndani zaidi ambayo Francis mwenyewe anaiambatanisha
na umaskini.
Mtu yeyote hapaswi kushangaa kwamba Francis anaongea sana juu
ya hali ya umaskini, kwani yeye mwenyewe ni mwenyeji wa Amerika ya Kusini: sehemu
ya ulimwengu ambapo mamilioni ya watu (isipokuwa Chile) wanaishi kwenye umaskini mkuu.
Utakuwa umekosa utu usipoguswa na tofauti za kutisha kati ya Recoleta ambao ni mji
mzuri na wa kupendeza wa Buenos Aires, unao ufanya mji huo kujulikana kama Paris ya
Kusini, na hali duni ya maisha ya vitongoji kama vile Rodrigo Bueno. Wakristo hawana
budi kuguswa na tofauti kama hizi. Lakini ili tuyaelewa maneno ya Francis juu ya umaskini
lazima tuelewe kwamba Baba Mtakatifu ni Mkatoliki haswa. Yeye sio mwanafalsafa au
mchumi mtendaji (practical materialist). Kwa hivyo, ung’amuzi wa Papa Francisko juu
ya maskini na umaskini unapita ule uelewa wa kawaida wa kijamii kuhusiana na maswala
haya.
Katika cha kusisimua cha maswali na majibu kwenye vigilia ya Pentekoste
ya mwaka huu, pamoja na washiriki wa vyama vipya katika Kanisa (new movements) ambavyo
vimechangia sana kuleta uhai ndani ya Kanisa tangu Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican,
Baba Mtakatifu aliyasema haya kuhusu Ukristo na Umaskini.
Kwetu Wakristo umaskini
sio swala la kijamii, kifalsafa au kitamaduni. La hasha, bali ni swala la kiteologia.
Ningesema pengine swala la kwanza, kwani Mungu Mwana alijishusha, akajifanya maskini
ili kuweza kuambatana nasi kwenye njia yetu. Na huu ndio umaskini wetu: umaskini wa
mwili wa Kristo, umaskini ambao mwana wa Mungu alituletea kwa kujifanya mtu kwake.
Kanisa maskini kwa ajili ya maskini linaanza kwa kuuelekea mwili wa Kristo. Tukiuelekea
mwili wa Kristo, tutaanza kuelewa kitu, kumbe tutaelewa maana hasa ya umaskini huu,
umaskini wa Bwana.
Kwa neno moja, hili linagusia unyenyekevu. Kama Myesuiti
mwingine, Philip Caraman, alivyoandika wakati mmoja, unyenyekevu ni fadhila “ambayo
kwayo tunajipima kisawasawa mbele ya Mungu, tukitilia maanani yote yale ambayo Mungu
ametupa, ametufanyia, na anayotarajia kutoka kwetu.”
Uelewa mwingine unatokana
na kukumbuka kwamba neno la Kigiriki lililotumiwa kwenye Injili ya Mathayo(5:3) kuelezea
“umaskini wa kiroho” (πτωχός) lina maana ya kushushwa hadi kuwa mwombaji. Kwa sababu
hiyo, maskini wa kiroho ni wale kati yetu – maskini, tajiri, wenye kipato cha kati
– wenye kuzifahamu dhambi zetu na kumwomba Kristo atuokoe.
Hiki ndicho kiini
cha nini hasa maana ya Kanisa Maskini. Kanisa nyenyekevu sio Kanisa lenye uoga, lenye
waumini wenye kunyong’onyea kwenye mambo ya imani; bali ni Kanisa ambalo linawajumuisha
watu ambao, kwa uhuru kabisa, wanajitoa kidete kwa Kristo aliye peke yake mwenye uwezo
wa kutuokoa.
Hayo pia yanajiri kwenye tafakari juu ya maisha ya Mtakatifu Francisko
wa Assisi. Hapa ni vizuri kuonesha pengo lililopo kati ya riwaya zisimuliwazo juu
ya Francisko, na ukweli hasa juu ya mtu huyu.
Kwa mfano, katika wake wa hivi
karibuni juu ya Francisko, Mdominikani Augustine Thompson, anaonyesha kwamba mazungumzo
yaliyosifika sana kati ya Francisko na Sultan al-Kamil wa Misri hayakuchangiwa na
hisia zozote au harakati dhidi ya vita. Kwake Francisko, lengo la tendo hili lilikuwa
kumbadilisha Sultan huyo kuwa Mkristo!
Pia Thompson anaonyesha ukosefu wa subira
wa Francisko juu ya ulegevu kwenye maswala ya Kiliturjia, ukosefu wake wa kujihusisha
na aina yoyote ile ya programu za kisheria au mageuzi ya kijamii, uwezo wake wa kubainisha
kati ya umaskini hohe hahe na ule wa kawaida, na pia hakushikilia itikadi na fikira
zilizojiri kwa wakati wake kuhusiana na Mungu na Mazingira au Pantheism kwa lugha
ya Kimombo; na kwamba kitu asichokuwa akitazamia kabisa Francisko ni kwa shirika lake
kugeuka kuwa kikundi cha wafanyakazi wa kijamii au social workers. Mtakatifu Francisko,
anaendelea kusema Thompson, alikuwa mkakamavu wa imani, na kwamba Francisko alikuwa
mtii kwa Mungu na Kanisa, akimaanisha uongozi wake mathubuti.” Katika wosia wake wa
mwisho, Fransisko hata alisisitiza kwamba waasi au wakiukaji wa sheria ambao wangejitokeza
kwenye shirika lake watolewe kwa serikali ili iwashughulikie kulingana na sheria za
nchi.
Kutokana na yote haya, inakuwa vigumu kumwona Francisko kama mpinzani,
au mtetezi na mwanaharakati wa namna yoyote ile. Hata Wakatoliki wengine hushangaa
wanapogundua kwamba uelewa wa Francisko juu ya umaskini haukuwa unapinga tofauti za
kijamii juu ya kipato au kuwaonea wivu matajiri. Thompson anaonyesha kuwa Mtakatifu
huyu aliandika kidogo sana juu ya umaskini, na wakati alipoandika, haikuwa na uhusiano
na “kujibandua kabisa na mali, maisha ya kawaida, au kuishi tu kwa siku hiyo.” Bali
ilikuwa hasa kuhusiana na ukweli kuhusu Nafsi ya Pili ya Utatu Mtakatifu aliyejishusha
na kuchukua hali ya kibinadamu katika umwilisho na kujitoa sadaka kwa ajili ya binadamu
wote kwa kufa Msalabani.
Kwa hiyo, kulingana na Thompson, mtazamo wa Mtakatifu
Francisko kuhusu umaskini ulikuwa hasa ni “kujikana mwenyewe, kutoa huduma kwa ajili
ya Mungu na kuyatii Maandiko Matakatifu yanayohubiriwa na Kanisa la Kristo. Kwa maana
hiyo, mawazo ya Francisko kuhusiana na umaskini, kama alivyoandika Thompston , siyo
ya “kisiasa.” Ila ni kuhusu kuufikia utajiri wa kiroho unaotokana na kumkumbatia hasa
Kristo.
Je, hili linatuambia nini kuhusiana na jinsi wakatoliki wanapaswa
kuwaza juu ya umaskini? Kwanza kabisa, ukereketwa wa kisiasa usiwe ndicho kitu
cha kwanza kufikiria tunapoongea juu ya kukomesha umaskini. Sio bure kwamba Baba Mtakatifu
Francisko kwenye mahubiri yake ya vigilia ya siku ya Pentecost alisisitiza kwamba
“Kanisa sio mfumo wa kisiasa, au chama fulani, na kwamba kama Kanisa... sisi si Shirika
lisilo la Kiserikali (NGO), na kwamba, Kanisa linapokuwa NGO, linapoteza chumvi na
ladha yake, na hivyo linabaki kama chama tu, bila uhai.”
Ni kweli kwamba
wa Baba Mtakatifu Francisko kwa serikali kuzingatia majukumu yao hasa kuhusiana na
maswala ya uchumi wa kimataifa, unatokana na uhakika wake kwamba kuna jukumu la kisiasa
katika kukabiliana na umaskini. Ila maandishi yake kabla ya kuchaguliwa kuwa Papa
yanabainisha kwamba Francisko analiona hili kwani hapo 2011 (wakati uchumi wa Argentina
ulipoanguka), Bergolio aliandika kwenye jarida la , kwamba “kuna waagentina wanaokumbwa
na umaskini na kusukumwa pembezoni mwa jamii, ambao ni lazima tuwachukulie kama wadau
na wahusika katika kuchonga hatima ya maisha yao wenyewe, na sio tu kama wafaidi wa
misaada inayotolewa na serikali na mashirika ya kijamii”.
Lakini zaidi ya yote
Francisko anawataka wakatoliki kuonyesha mwanga wa kikristo katika kukabiliana na
swala la umaskini. Katika hotuba yake ya vigilia ya Pentekoste, alisisitiza kwamba
lengo letu la kwanza lisiwe nguvu tendaji na kufanikiwa. “Ni kitu kimoja kumhubiri
Yesu,” Francisko aliwaambia wasikilizaji wake, “na kitu kingine kufanikiwa.”
Haimaanishi
kwamba wakristo hawana wajibu wa kufikiri na hata kujadiliana jinsi ya kuukomesha
au kuupunguza umaskini. Ndivyo inavyodai haki. Francisko anataka kutuonyesha kwamba
ikiwa tutashughulikia tu “mafanikio kwa mtazamo wa kidunia”, kuna hatari ya kuusahau
upendo wa Kikristo.
Katika kuendeleza mjadala wake, Papa Francisko aliwauliza
maswali mawili wale waliokuwa wakimsikiliza: “Niambieni, unapomsaidia mtu aneyeomba
njiani, unamwangalia machoni baba au mama huyo?. . . Na unapomsaidia, unamshika mkono
unayemsaidia au unamrushia tu vishilingi?” Mambo matatu—kama asemavyo Francisko!—yanajitokeza
hapa. Moja ikiwa ni: mara ngapi sote tumeanguka mtihani huu?
Pili ni Mwenyeheri
Theresa of Calcutta. Hakuwa na mawazo ya kufanikiwa alipoamua kuwahudumia walio hoi
zaidi miongoni mwa watu wa dunia. Katika maisha yake, alikaripiwa kwa kutokujihusisha
zaidi kisiasa kuhusu baa la umaskini. Ila kazi yake haikuwa ya kisiasa. Ilikuwa juu
ya kitu ambacho ni kikuu kuliko siasa: kuuleta upendo wa Kristo kwa wale ambao Kristo
mwenyewe alituambia tutauona uso wake ndani mwao.
Na tatu ni kile ambacho
Papa mstaafu Benedicto XVI alisisitizia sana kwenye waraka wake wa kwanza wa kipapa,
, Mungu ni Upendo. Ijapokuwa waraka huu ulisisitiza sana maswala ya haki, Benedict
wa kumi na sita alikazia kwamba kuna kitu ambacho kila mtu anayekumbwa na mateso anakihitaji
zaidi: “upendo wa kipekee na kuthaminiwa.”
Kwao Baba Mtakatifu Francisko, mtangulizi
wake (Benedikto wa kumi na sita), na Mwenye heri Mama Theresa (Wa Calkutta), jibu
letu kuhusiana na umaskini lazima liwe, juu ya yote, kuonyesha haswa huruma, ambayo
ndiyo kiini cha Injili. Pamoja na mambo mengine, hii inasaidia kusahihisha ule mwelekeo
wa kibinadamu kwamba haki tu inatosha. Mungu angekuwa ni Haki tu, bila Upendo asingeweza
kushuka na kuingia kwenye historia ya wanadamu kwa umbo la Yesu Kristo ili kutuokoa
kutokana na sisi wenyewe. Tulikuwa hatumdai Mungu chochote. Kwa maana hiyo, basi,
uelewa wa Kikatoliki kuhusu umaskini unatukumbusha kwamba ni Huruma ya Kimungu, na
sio haki, ambayo inatuokoa. Imehaririwa na Sista Brigita Samba Mwavasi