2013-10-13 13:34:08

Papa Francisko aiweka wakfu dunia kwa moyo Mtakatifu wa Maria Mkingiwa dhambi ya asili


(Vatican Radio) Mapema Jumapili hii 13 Oktoba , Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya maadhimisho ya Siku Kuu ya Mama Yetu wa Fatima. Ibada iliyohudhuriwa na mamia ya maelfu ya waamini, mahujaji na wageni. Baada ya Ibada ya Misa Papa aliongoza pia sala mbele ya Sanamu asilia ya Mama Yetu wa Fatima, na kisha aliiweka wakfu dunia, kwa Moyo Mtakatifu wa Maria mkingiwa dhambi ya asili, Mama wa Mungu.

Maadhimisho ya Siku Kuu hii Vatican, yamepambwa zaidi na uwepo wa sanamu hii asilia ya Mama Yetu wa Fatima, iliyosafirisha toka makazi yake huko Fatima Ureno hadi Vatican siku ya Jumamosi 12 Octoba 2013, kama sehemu ya matukio ya Jimbo la Roma kaatika kuuadhimisha Mwaka wa Imani.

Jumamosi maelfu ya waamini, mahujaji na wageni pia walikusanyika katika uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya kuungana na Papa Francisko , kutoa heshima zao kwa sanamu asilia ya Mama yetu wa Fatima.

Sanamu hiyo , Jumamosi , iiliingia katika uwanja wa Mtakatifu kwa Maandamano ya kupendeza, yaliyoongozwa na maaskari walinzi wa Papa, na kisha Papa aliwaongoza waumini kusali matendo saba ya uchungu ya Maria. Na kutoa homilia yake ambamo alieleza zaidi juu ya imani ya Bikira Maria , Mama wa Imani , kwamba, imani yake ni pingu ya dhambi.

Dhambi , alisema, ni aina ya pingu inayotengenezwa ndani mwetu , pingu yenye kutuondolea amani na utulivu ndani mwetu. Na “ndiyo” ya Bikira Maria, kwa Malaika Gabriel, iliyoufungua mlango kwa Mungu kufungua pingu ya dhambi ya asili ya ukosefu wa utiii. Maria ni mama, ambaye kwa uvumilivu na upendo, anatuleta sisi kwa Mungu, ili tuweze kufungua pingu zinazofunga mioyoni yetu.

Papa pia aliendelea kutafakari jinsi imani ya Maria iilivyo mwilisha mwili wa Yesu. Na hivyo kuamini katika Umwilisho , anasema, ina maana ya kumpa mwili wetu Yesu , kwa unyenyekevu na ujasiri wa Maria , hivyo kwamba anaweza kuendelea kukaa katikati yetu.

Kisha Papa alizungumzia safari ya imani ya Maria, akisema , yeye ni hututangulia na kutudumisha daima katika safari hii ya iman. Daima Maria huambatana na nasi katika safari ya kumfuata mwanae. Maria alielewa kwamba, safari ya imani ni kupita katika njia ya msalaba tangu mwanzo wake, kama ilivyokuwa tangu Herode akitaka kumuua Mtoto Yesu, mpaka mateso yake na kifo chake msalabani .


Maria alipopata habari kwamba kaburi lilikuwa tupu , moyo wake ukajaa furaha katika imani . Imani katika kristo, katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. Papa Francisko alihitimisha hotuba yake kwa kuigeukia Sanamu ya Mama yetu wa Fatima , akisema: Mama asante kwa kutuimarisha pia sisi atika imani . Na leo tunarudia kuidhaminisha kwako imani yetu, Wewe uliye Mama wa Imani yetu.








All the contents on this site are copyrighted ©.