Kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Bikira Maria -Roma, Jumapili 13 Oktoba 2013,
Papa Francisco ataongoza Ibada ya Misa ya Ekaristi kwa nia ya kuomba ulinzi na maombezi
ya Mama Maria Mtakatifu Sana wa Fatima , kwa ajili ya kanisa la ulimwengu na dunia
kwa ujumla .
Kwa ajili hii Sanamu asilia ya Mama Yetu wa Fatima, imeletwa
kwa mara ingine Roma, pia kama sehemu ya maadhimisho ya matukio ya Jimbo la Roma
kwa Mwaka wa Imani .
Sanamu ya Mama Yetu wa Fatima , inawasili Jumamosi hii
jioni tokea Fatima, na itapokelewa Vatican Papa Francis wakiwepo pia Askofu Mkuu
Rino Fisichella , Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Uinjilishaji Mpya.
Na pia waamini na maelfu ya waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa kanisa
kuu la Mtakatifu Petro kutoa heshima zao kwa Mama Yetu wa Fatima.
Sanamu ya
Mama Yetu Fatima mara ya mwisho, iliondoka katika makazi yake Fatima Ureno, wakati
wa Maadhimisho ya Jubilee Kuu ya miaka elfu mbili ya Ukristu, kwa agizo la Mwenye
Heri Yohane Paulo 11, tarehe 13 Mei kama ishara ya kuweka maisha yake yote chini
ya ulinzi wa Mama Maria. Jumamosi akitoa maaelezo kwa waandishi wa habari, Askofu
Mkuu Rino Fisichella, alikumbuka mapenzi makubwa aliyokuwa nayo MwenyeHeri Karol
Wojtyla,kwa Mama Yetu wa Fatima, ambaye alipenda tarehe siku aliyopigwa risasi na
kujeruhiwa hapo Mei 13 , 1981, aweke taji kwa Sanamu ya Mama Yetu wa Fatima, aliye
watokea watoto watatu wa Fatima Ureno. Mwenye heri Yohane Paulo 11 , aliamini ni Mama
Yetu wa Fatima, ndiye aliyemwokoa na shambulio hilo. Na hivyo alijiweka chini ya ulinzi
wa Mama yetu wa Fatima, kama mlinzi na mwombezi wake. Katika maisha yake yote. . Na
kwamba katika muda wa siku hizi mbili, Sanamu ya Mama Yetu wa Fatima, ikiwa Roma
na Vatican, kama kawaida, waamini watafanya hija katika Kaburi la Mtakatifu Petro
, na kusikiliza Katekesi ya Papa atakayoitoa katika Uwanja Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro .
Baada ya kuwasili Vatican, kutoka Fiumicino , sanamu ya Mama yetu
wa Fatima, itapelekwa katika kanisa dogo la Monesteri anakoishi Papa Mstaafu Benedict
XVI, ambako atafanya sala binafsi kwa muda mfupi. Na baadaye Sanamu itapelekwa katika
Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ambako itapokelewa na Papa Francisko. Na baadaaye
sanamu itapelekwa kwa Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, ikiwa imebebwa na waumini
wa kujitolea , chini ya ulinzi na usimamizi wa jeshi la “The Swiss guards” na polisi
wa na polisi Vatican. Na kisha sanamu itapelekwa katika madhabahu ya Maria ya Upendo
wa Mungu yaliyoko nje kidogo ya jiji Roma,”Divino Amore” ambako kutakuwa na Ibada
ya Rozare Takatifu na mkesha wa maombi na sala . Jumapili sanamu inarudi katika
uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Ibada ya Misa ya Ekaristi itakayoongozwa
na Papa, kwa nia ya kulikabidhi Kanisa katika ulinzi na maombezi ya Maria