Washiriki wa Mkutano wa Pamoja wa Vyama na Mashirika ya Biblia wakutana na Papa Vatican
Jumatano baada ya katekesi yake kwa mahujaji na wageni, Papa Francisko, alikutana
na washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Vyama vya Biblia na Shirikisho la Biblia Katoliki,
ambao wamekuwa pamoja kufanya mkutano wao wa kwanza hapa Roma. Mkutano uliofanyika
chini ya uongozi wa Askofu Mkuu Vincenzo Paglia , ambaye ni Rais wa Shirikisho la
Katoliki Biblia na Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya familia.
Pamoja na
kupitia upya mipango iliyoandaliwa na makundi yote mawili ya kukuza kujifunza Biblia
katika kila pembe ya dunia , washiriki pia, walijadili juu ya Sinodi ya Maaskofu
iliyotangazwa hivi karibuni na Papa juu ya Familia ambayo itafanyika Oktoba 2014.
Mkutano
wa wiki wa vyombo hivyo viwili, umetoa nafasi nzuri ya majadiliano kwa washiriki
wanachama wa UBS na CBF, na wamewasilisha kwa Papa Francisko, nakala za Biblia tofauti,
zilizo chapishwa katika miaka ya hivi karibuni, nakusambazwa pande mbalimbali za
dunia. .