2013-10-11 09:44:20

Papa Francis: tunampokea Mungu Mwenyewe katika ujasiri wa sala!


Katika sala ni lazima kuwa na ujasiri wa kuigundua neema ya kweli, inayotolewa kwetu na Mungu Mwenyewe. Huo ulikuwa ni ujumbe wa Papa, wakati wa Ibada ya Misa asubuhi siku ya Alhamisi, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta .

Katika moyo wa mahubiri yake, Papa alilenga katika uwepo wa Yesu , katika Injili ya siku, tunapoomba kwa msisitizo na kuamini. Papa alieleza na kutaja mfano wa rafiki muhitaji, aliyeng’ang’ana kuomba msaada wa rafiki yake , ambaye hatimaye aliamuka na kumpatia alichokuwa akihitaji , hivyo shukurani kwa msisitizo wake .
Papa Francisko, aliendelea kutafakari juu ya ubora wa sala zetu, akisema, mfano uliotajwa katika Injili, unatupa sisi nafasi ya kufikiri , ni jinsi gani tunaomba? Je, tunaomba kwa imani na saburi na msisitizo , au tunasali tu kama mazoea ya kila siku bila ya kuwa makini katika kile tunachokiomba? Na je tunajiweka kwa ujasiri mbele ya Bwana kuomba neema, wakati tunaopoomba mahitaji yetu ? Maombi yasiyokuwa na ujasiri, hayo si maombi ya kweli. Katika ujasiri wa imani, Bwana hutusikiliza . Ni kuwa na ujasiri na kubisha juu ya mlango, kama . . Bwana alivyosema: Kwa maana kila aombaye hupewa, na atafutaye , hupata; na abishaye , atafunguliwa. Hivyo tunapaswa kuomba, kutafuta, na kubisha.

Papa aliendelea kutafakari iwapo kweli tunazama ndani ya maombi . Naa kama tunajua kubisha hodi juu ya mlango wa moyo wa Mungu. Kama ndivyo , kama Yesu alivyofundisha , ikiwa ninyi waovu mwajua kuwapa zawadi nzuri watoto wenu, ni mara ngapi zaidi Baba wa mbinguni atawapa Roho Mtakatifu ? Papa anasema hili “ jambo Kubwa”.

Aliendelea kusema, wakati tunaomba kwa ujasiri, Bwana anatupa neema, na pia anatupa Mwenyewe neema ya Roho Mtakatifu , ambaye ni yeye Mwenyewe! Bwana kamwe hatupi neema zake kwa njia za barua pepe , lakini yeye mwenyewe hutukabidhi kile tunachokiomba kwa ujasiri wa imani. Hutuletea mwenyewe kile tunachokiomba, ni bahasha ya neema iliyofungwa , neema ya kweli ambaye ni Yeye, anakuja na kutuletea. Maombi yetu , yakifanyika kwa ujasiri, tunapata kile tunachokiomba,na Mungu anajua kilicho muhimu zaidi kwetu.

Papa alibaini katika Injili baadhi ya watu walipokea neema na kisha kwenda mbali kama ilivyokuwa katika kundi la watu kumi wenye ukoma walioponywa na Yesu, ni mmoja tu aliyerudi mara moja kumshukuru. Na pia kipofu wa Yeriko baada ya kuponywa na Bwana, alimsifu Mungu. Hivyo tunafundishwa kwamba, ni lazima kuomba kwa ujasiri wa imani, na mara Bwana anapoyafanikisha yale tunayoomba ni lazima kumshukuru na kumsifu kwa huruma yake .
Papa alimazia akisisitiza , tunaomba neema, lakini hatuwezi kuthubutu kusema, njoo kwangu Bwana. Tunajua kwamba neema daima huletwa naye Bwana mwenyewe. Na hivyo tusijifadhaishe wenyewe kupokea neema, bila ya kutambua kwamba imeletwa na yeye Mwenyewe kwetu. Na tusali kwa ujasiri na utambuzi kwamba, Bwana hutupatia neema yeye Mwenyewe, daima, katika neema ya kila hali. Na tupate kumtambua , na kumsifu, kama walivyofanya watu wagonjwa walioponywa katika Injili. Na hivyo kwamba , katika neema, tuweze kukuta Bwana.








All the contents on this site are copyrighted ©.