Maoni ya Askofu Mkuu Michael Fitzgerald juu ya Hati ya Kichungaji ya amani duniani.
(Vatican Radio)Katika Waraka wa Kitume wa Papa Yohane XXIII, juu ya Amani Duniani(Pacem
in Terris) mna kanuni muhimu ya uhuru wa dini, ukionyesha umuhimu wa mwendelezo wa
mahusiano kwenye mchanganyiko wa dini leo hii. Hayo ni maoni ya Askofu Mkuu Michael
Fitzgerald , aliyekuwa Mjumbe wa Papa Misri na Rais wa zamani wa Baraza la Kipapa
kwa ajili ya Mazungumzano kati ya Dini.
Askofu Mkuu Fitzgerald, alitoa maoni
hayo wakati akizungumza na Philipa Hitchen wa Radio Vatican , wakati akiwa Roma kuhudhuria
mkutano wa hivi karibuni, kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya barua ya Papa Yohana
XXIII , Pacem in Terris.
Katika mahojiano, Philippa Hitchen alitaka kujua
iwapo hati ya Papa Yohane XXIII aliyoiandika wakati wa vita baridi, inaweza kusaidia
wale wanaofanya kazi ya kukomesha madhulumu ya kidini duniani kote leo hii. Na Askofu
Mkuu Fitzgerald, kwanza alionya kwamba, hati hiyo haitoi hukumu kwa madhulumu yaliyokuwa
yakifanyika dhidi ya Wakristu, lakini inatazama zaidi hoja ya matendo mema kama msaada
katika kufanikisha mema kwa wote.
Na kwamba, kuna kanuni ya uhuru wa dini,
hasa katika utendaji wa dini wa mtu , katika maisha yake ya kila siku, si tu katika
maisha ya binafsi au umma kwa ujumla lakini pia katika , na uhuru wa dhamiri na imani
ili kwamba mtu anaweza kubadili dini yake kama dhamiri yake inavyomtuma, jambo linaloleta
matatizo hasa katika ulimwengu nchi nyingi za Kiislamu . Aidha kuna sheria potofu
zinazo zuia ujenzi wa maeneo ya ibada kama makanisa au misikiti au watu kushiriki
katika ibada mahali popote. Askofu Mkuu Michael anasema , huko ni kuwa kinyume na
misingi ya haki za binadamu. Katika vikwazo hivyo, inabidi kutafuta jawabu kupitia
njia ya mazungumzano, hasa yanayolenga katika kuelewa maana ya haki za binadamu na
kutekelezwa inavyopaswa. Askofu Mkuu Fitzgerald, alieleza na kuonyesha kufurahia
kwamba, kumekuwa na ishara nzuri za kutia moyo .... kama hatua iliyochukuliwa na Taasisi
maarufu ya dini ya Kiislamu la Misiri Al-Azhar , kuruhusu masheikh na maimamu kushiriki
katika mkutano wa Roma, ambako kwa pamoja wameweza kuuona mtazamo wazi wa mwelekeo
wa dini nyingine, hivyo hiii imekuwa ni fursa ya kutafsiri katika hatua za kawaida
na msaada wa kupanua uelewa kwa Waislamu na kwa Wakristo pia kuona hakuna sababu za
kushambuliana kwa sababu za kidini. Bali dini inapaswa kuwa chombo cha kukuza amani
na maelewano.