2013-10-09 07:49:51

Mkutano waandaliwa juu ya watu na misingi ya maisha ya kijamii


Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia , katika maadhimisho ya kutimia miaka 30, tangu kutolewa kwa Hati ya haki za Familia , Baraza limeandaa Mkutano utakaoongozwa na Mada: Mwelekeo mpya wa kijamii na haki za Familia . Mkutano huo utafanyika hapo 24 Octoba mjini Roma katika jengo la Domus Pacis.

Rais wa Baraza la Familia Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, atafungua mkutano huo.Kipindi cha kwanza cha Mkutano kitaongozwa na Kardinali Luis AntonioTagle wa Manila Ufilipino. Nyakati za mchana, mkutano utaongoza na Kardinali John Olorunfemi wa Jimbo Kuu la Abuja , Na Katibu wa Shirika Mons. John Laffitte, atazungumzia mahusiano katika misingi ya kiteolojia akiainisha na Hati ya Haki za binadamu.
Wengine watakaoshiriki katika mkutano huu ni pamoja na mwanafalsafa na mwanasheria Andrés Ollero ,Pia Mkuu wa Chama cha Knights ya Columbus, Carl Anderson , akiwempo pia profesa Jane Adolphe , na Mchumi Stefano Zamagni.
Waandaaji wa mkutano wanautaja Mkutano huu, kuwa fursa muhimu ya kujadiliana ukuaji si tu kwa kanisa, bali pia maisha ya kijamii na kiraia. Na hivyo inatarajiwa kuwa wa manufaa kwa washiriki na watazamaji.

Kwa ajili hiyo , Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia , linawaalika wote wanaopenda kuwa mtazamaji katika mkutano huu, kutuma barua pepe kwa: . barua zitapokelewa hadi Ijumaa 18 Octoba 2013.








All the contents on this site are copyrighted ©.