2013-10-09 15:28:17

Jimbo la Kondoa kuweka wakfu Kanisa lake kuu


JImbo la Kondoa nchini Tanzania, linajiandaa kuliweka wakfu Kanisa Kuu la jimbo wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Paulo wa Msalaba, hapo tarehe 19 mwezi October, 2014.

Akiongea hivi karibuni na mtandao wa habari wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Afrika mashariki nay a kati, AMECEA, Askofu Bernardini Mfumbusa wa jimbo la Kondoa amesema kwamba jimbo liko kwenye harakati za mwishomwisho katika ujenzi wa Kanisa hilo kuu la Roho Mtakatifu, na kwamba hapo mwakani litakuwa tayari kuzinduliwa kirasmi.



Jimbo la kondoa lilianzishwa mnamo mwaka 2011, na lilimegwa kutoka jimbo la Dodoma.



Askofu Mfumbusa anawashukuru wote waliofanikisha ujenzi wa kanisa hilo, huku akisema majimbo mengine kama vile Arusha Dodoma na Dar – es – Salaam yalichangia kiasi kikubwa kwenye ujenzi huo. Amewashukuru waumini wa majimbo hayo, wakiwa ni walei, watawa na mapadre waliojitolea kidete kuona kwamba jimbo lina Kanisa Kuu.

Pia ameyashukuru mashirika yaliyochangia kwenye ujenzi wa kanisa hilo kama vile Propagada Fide, (Vatican), Missio-Munich, (Germany); Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, (USCCB) Solidarity Fund for Africa, Kirche in Not, Wamissionary wa Mtakatifu Peter Clavery, na Jimbo la Bolzano-Bressanone (Italy).

Jimbo la Kondoa lina waumini WasioMpaka kumalizika, Kanisa kuu la Roho Mtakatifu la Kondoa litakuwa limetumia Tsh. 816,000,000 (sawa na Euro 388,571.) Kondoa ndilo jimbo dogo zaidi Tanzania, likiwa na waumini wa kikatoliki 50,000 kati ya wakaaji 450,000 wa wilaya hiyo.

chanjo: AMECEA Social Communication office










All the contents on this site are copyrighted ©.