Viongozi wa Africa wahimiza kusitisha watu kuhama nchi zao
AskofuMkuu Berhaneyesus Demerew Souraphiel wa Addis Ababa, akizungumza na Redio Vatican
mwishoni mwa wiki alisema , viongozi wa Afrika wanapaswa kuona ni fedheheshwa na aibu
kwao kushindwa kufanikisha amani, uhuru,demokrasia , nafasi za kazi na maisha ya
kuvutia kwa watu wao. Askofu Mkuu huyo aliasa, kwa kurejea tukio la wiki iliyopita
katika kisiwa cha Lampedusa , ambako vimetokea vifo vilivyotisha dunia, kwa wahamiaji
karibia mia mbili, waliokuwa wamepania kuingia Ulaya toka Afrika, kuzama maji.
Aidha
Askofu Mkuu wa Addis, amezitaka pia serikali za Ulaya, kuboresha sera zao za uhamiaji
na taratibu wakimbizi, wanaoomba idhini za kuingia katika nchi zao, kama inavyotakiwa
na sheria za Umoja wa Mataifa, ili kulinda haki za binadamu. Hata hivyo, aliongeza,
serikali za Afrika lazima kuboresha hali ya uchumi na huduma kwa jamii, kiasi kwamba
wananchi wasione haja ya kuhatarisha maisha yao kwenda nchi za mbali kutafuta maisha
ahueni, na tamaa zisizo na kipimo katika kutafuta mali .
Aidha Askofu Mkuu
Berhaneyesus amemetoa wito kwa vijana wa Afrika, kuwa na ujasiri wa kubaki katika
bara lao na kufanya kazi pamoja ili kuboresha hali halisi ya Afrika kuliko kutoka
nje ya Afrika, alisisitiza katika maelezo yake wakati akihojiwa na Padre Moses Hamugole
wa Radio Vatican.