Siku ya upashanaji habari duniani ya mwaka 2014, inaadhimishwa kwa lengo la kutazama
kw amakini zaidi, uhusiano kati ya mawasiliano na utamaduni wa mahusiano. Hii ni inaashiriwa
na mada iliyotolewa mwishoni mwa wiki kwa ajili ya siku ya upashanaji habari duniani.
Mada yenyewe ni: Mawasiliano katika huduma ya mahusiano ya kweli ya tamaduni. Kulingana
na Kamati ya kipapa kwa ajili ya mawasiliano ya kijamii, binadamu hujieleza na kuendeleza
mahusiano yake kwa njia ya mawasiliano. Uwezo wa kuwasiliana vyema unahitaji unyofu,
uadilifu, unyenyekevu na heshima kwa wengine; pamoja na nia na jitihada ya kuweza
kujifunza kutoka kwa wengine. Zaidi ya yote, mawasiliano ni maarifa yanayohitaji mazungumzo
na majadiliano katika ukweli. Ni katika kufanya hivyo ambapo binadamu ataweza kutambua
kumbe tofauti zilizomo kati ya watu ni utajiri mkubwa kwa jamii ya binadamu. Na katika
kutambua jambo hilo, mwanadamu pia anatambua na kuelewa ukweli sio tu wa wengine,
hata zaidi, ukweli juu ya nafsi yake mwenyewe. Dunia kwa sasa hivi inapitia utamaduni
mpya, linasema gazeti la kila siku la Osservatore Romano, lenye kuchpishiwa mjini
Roma. Utamaduni huo mpya unaendelezwa na teknologia, na hivyo mawasiliano yamepanuliwa
na yanaendelea kukua na kupanuka. Ni mwaliko kwa jamii nzima kuendeleza mawasiliano
ndani ya mtazamo mpya, kwamba licha ya mahusiano ya kibinafsi, mawasiliano hutoa pia
nafasi muafaka kwa jamii nzima kuweza kuonja utamu na urembo wa kutembea pamoja kama
jamii ya kizazi kipya, kwenye safari ya maisha na safari ya kiroho. Urembo wa kiimani
na hata wa kukutana na Kristo, kama alivyobainisha baba mtakatifu Francisko alipokuwa
akiongea na waliohudhuria mkkutano wa hivi karibuni wa Kamati ya kipapa kwa ajili
ya mawasiliano ya kijamii, uliofanyika mjii Roma na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi
za juu wa Kanisa kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Hivyo Tema ya siku ya upashanaji
habari duniani mwaka 2014 inatoa changamoto na inawaalika wote wenye kujihusisha na
mawasiliano ya kijamii kuzingatia ukweli, usahihi na uthabiti wa yale wanayowasilisha
kwenye jamii, huku wakizingatia maadili na imani yao ya kikristo wanayoiishi ndani
ya tamaduni mambo leo. Huu ni mwaliko pia wa kuzingatia lugha mwafaka kwa ajili ya
kuyafikia malengo ya mahusiano na ushirikiano kwenye jamii. Uwezo wa kuwasiliano
unaonekana kwenye ubunifu katika kuafikia ushirikiano na upendo katika mwuungano kama
ule wa utatu mtakatifu; ambayo ni zawadi inayowasaidia watu kukua katika mahusiano
binafsi, na kuendeleza majadiliano kama jibu muafaka dhidi ya utengano unaoletwa na
chuki, uhasama na migogoro ndani ya jamii na kati ya mataifa. Ulimwengu wa utandawazi
unaashiria kasi ya uwezo wa mawasiliano kufikia kona zote za dunia, za ulimwengu halisi;
unaashiria pia kasi hiyo hiyo ya mawasiliano kwenye ulimwengu “ulioumbwa” na tecknologia;
ulimwengu wa mitandao ya kijamii. Hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha uwepo wa mawasiliano
bora hata kwenye mitandao ya kijamii na kuendeleza usikivu, majadiliano ya kina na
matumaini, kama anavyopendekeza Papa, ili kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma
katika kuendeleza mahusiano mema na mawasiliano ndani ya jamii. Ujumbe unaotolewa
na mada ya siku ya upashanaji habari duniani kwa mwaka 2014 inatafuta kuchunguza ukuu
wa mawasiliano kwenye ulimwengu ambao unaendelea kwakaribia watu wake zaidi na zaidi
kwa njia ya mitandao, ili kuhakikisha kwamba mitandao hiyo inarahisisha na kuboresha
mahusiano na ukaribianaji wa watu kwenye ulimwengu unaozingatia haki na usawa zaidi
kwa watu wake. Siku ya upashanaji habari duniani ilianzishwa na Mtaguso Mkuu wa
pili wa Vatikani kupitia hati ya Inter Mirifica, na inaadhimishwa kila mwaka kwenye
Jumapili ya Pili baada ya Maadhimisho ya Pentekoste.