Siku ya Kimataifa ya kupinga vurugu,ukatili na mapigano
Jumatano, Oktoba 2, kwenye Umoja wa Mataifa, kuliadhimishwa Siku ya Kimataifa ya
kupinga vurugu na ukatili. Siku hii pia, India huadhimisha kumbukumbu ya siku ya
kuzaliwa kwa Mahatma Gandhi, mtu mashuhuri wa India , aliye eneza ujumbe wa kupigania
haki na uhuru bila vurugu au ghasia. Hafla Kkatika Umoja wa Mataifa iliandaliwa na
ubalozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki moon, akiwa mgeni rasmi, alitoa wito kwa watu wote duniani, wakubali kuongozwa
na roho wa kupenda wengine na kuikataa roho katili ya kudhuru wengine. Ban Ki Moon
alitoa rai hiyo, akitazamisha katika ushupavu na ujasiri wa Mahatma Ghandi, mtu mashuhuri
katika wajibu wa kutafuta haki kwa njia ya amani na kuvumiliana. . Tarehe 2 Octoba
,kila mwaka ilitengwa na Baraza Kuu la umoja wa Mataifa kwa ajili ya kueneza ujumbe
wa amani, kupitia elimu na ufahamu kwa umma. Balozi wa kudumu katika umoja wa
Mataifa toka India, Asoke Kumar Mukerji, alitoa ujumbe wake kwamba, âmazungumzo na
uelewano wa kutoandama vurugu umejitokeza kuwa chombo muhimu cha kisera, iwe ni katika
kutatua mizozo ya silaha au kutoa mkakati wa ukuaji na maendeleo, ni ulimbo unaowaunganisha
wanadamu, licha ya tofauti zao nyingi. Alisisitiza njia hii ya majadiliano bila
vurugu na kupingana, si tu inahusu kuubadili ulimwengu, bali pia kumbadili mtu binafsi.
Na Mahatma Gandhi daima alikumbusha kuwa majadiliano na mazungumzano katika hali ya
amani na utulivu , ni ndiyo njia ya watu jasiri, na wasio waoga. Hivyo ametaja kwamba
ni jukumu kupinga vurugu na ukatili, ili kusaidia kuweka dunia yenye amani kwa wote." Wawakilishi
wa nchi mbali mbali walitoa hotuba za kumuenzi Mahatma Gandhi na wengine kama Martin
Luther King Jr na Nelson Mandela, na kusisitiza haja ya kuepuka vurugu,ila kujenga
tabia ya kuvumiliana na kuendeleza mazungumzo ya amani.