2013-09-27 09:04:48

Warsha imeandaliwa kwa ajili ya maadhmisho ya "Pacem in Terris"


Wiki ijayo, baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani , limeandaa warsha ya siku tatu mjini Roma, tangu Jumatano 2 Oktoba 2013, kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya waraka wa Papa Yohane XXIII, juu ya Amani Duniani( “Pacem in Terris”). Madhumuni ya warsha hii ya siku tatu, ni kuchambua changamoto za sasa zinazoleta ugumu katika kufanikisha amani na maridhiano , kwa mwanga wa maono ya kinabii yaliyo ainishwa katika waraka wa Pacem in Terris .

Wajumbe watatazama tangu mgogoro wa Cuba hadi vita vya Syria, tangu tishio la vita baridi na changamoto za sasa zinazotokana na mitandao ya kigaidi ya kimataifa, na kwa jinsi wajibu wa upatanishi duniani ya leo hii, ulivyo badilika na kuwa mgumu kuliko ilivyokuwa miaka 50 illiyopita, wakati Papa Yohane XXII, alipo andika maoni yake, kwa dira mpya ya umoja na haki za binadamu kuheshimiwa kwa kila mtu binafsi.
Warsha inaunganisha pamoja wawakilishi wa kidini na kisiasa kutoka katika mabara matano, ikiwa ni pamoja na wasemaji kutoka Umoja wa Mataifa, Baraza la Ulaya, Umoja wa Afrika, na Shirika la Marekani Marekani .

Siku ya kwanza, washiriki watatazama jukumu la elimu Katoliki katika majiundo ya vijana kwenye uwezo wa kutekeleza utajiri wa kanisa, katika utamaduni wa haki, ndani ya mfumo mgumu wa kisiasa na kiuchumi.

Siku pa pili, ambamo Papa Francisko pia atashiriki, washiriki watalenga zaidi katika umuhimu wa waraka wa Pacem in Terris, katika mchakato unaoendelea kufanya mageuzi katika mashirika ya Umoja wa Mataifa , kwa ajili ya kukuza mshikamano zaidi wa amani kati ya watu na mataifa.

Siku tatu , warsha itatazama changamoto mpya katika ufanikishaji wa amani, ikiwa ni pamoja na kulinda haki za walio wachache kidini, na kukabiliana na vitisho dhidi ya maliasili na takataka za nyukilia na mgogoro wa sasa wa kiuchumi.

Inaelezwa msingi majadiliano yote, ni kuthibitisha kwamba, ukomo wa vita na migogoro haiwezi kupatikana hadi - kama Papa Yohane XXII alivyosema katika waraka wake wa Pacem in Terris, amani ipate kuwa na makazi ndani ya moyo wa kila mtu, wanaumme kwa wanawake. Na kama matokeo yake ya maafa ya vita baridi na mashindano ya silaha yanayoonekana, siasa ya uharibifu unaofanyika kila mahali, ni lazima ibadilishwe na sera za kuaminiana na ushirikiano wa pamoja kwa ajili ya mema ya wote.








All the contents on this site are copyrighted ©.