Mshikamano wa Makanisa na mashirika ya kijamii nchini Zambia (OASIS Forum), unaiomba
serikali ya Zambia kuwaruhusu wananchi wake kuchunguza mswada wa katiba kabla haujawasilishwa
bungeni na kupitishwa kama sheria kuu ya nchi hiyo. Hii itakuwa ni fursa kwa wana
Zambia kuhakikisha kwamba maoni yao yametiliwa maanani katika kurekebisha katioba
ya nchi hiyo.
Haya ni kwa mujibu wa ujumbe wa Oasis Forum kwenye vyombo vyahabari
vya nchi hiyo, siku ya jumanne (24/09/2013). Ujumbe huo uliotiwa sahahi na Padre Cleophas
Lungu ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia umetoa mwito kwa
uongozi wa serikali, wana kamati ya Katiba, na Waziri wa Haki wa Zambia kuonyesha
uzalendo wao na kuyafuata maadili ya katiba kuhusiano na utaratibu huo.
OASIS
Forum pia inasisitiza kuwepo kwa kipengele chenye kulinda utaratibu wa kutengeneza
Katiba, kwenye sheria za nchi hiyo. Ukosefu wa kipengele hicho, unasema ujumbe wa
OASIS Forum, unasababisha kutozingatiwa kwa taratibu na maadili yenye kuongoza shughuli
hiyo ya urabati wa sheria kuu ya nchi hiyo.
OASIS Forum ni kundi ambalo linayashirikisha
makundi ya kiimani na yale yenye kutetea haki jamii nchini Zambia. Wanachama wa OASIS
Forum ni pamojana Baraza la Makanisa, Zambia CCZ; Usharika wa Kiinjili Zambia, EFZ);
Baraza la Maaskofu Katoliki, Zambia, ZEC; Kamati kuu ya Mashirika yasiyo ya kiserikali,
NGOCC; na Umoja wa Wanasheria wa Zambia, LAZ.
OASIS Forum wamekuwa mstari wa
mbele katika kutetea utengenezaji wa katiba mpya nchini Zambia na kuhakikisha kwamba
shughuli hiyo inafanyika kwa njia wazi kabisa kwa manufaa ya wananchi wote wa Zambia.
Mshikamano huo pia umekuwa ukiwashauri wa Zambia kuungana kidete kwenye zoezi hilo
la kitaifa na kuhakikisha kwamba linafikia kikomo chake kwa amani.