Baba Mtakatifu Francisko, katika Katekesi yake kwa mahujaji na wageni, ameendelea
kuitafakari sala ya Nasadiki akisema, ndugu zangu wapendwa, katika sala ya Nasadiki
tunakiri kwamba Kanisa ni moja. Na tunapofikiri wingi wa utajiri wa lugha na utamaduni
wa watu waliomo katika Kanisa duniani kote , tunapata kuelewa zaidi kwamba umoja huu
wa kanisa ni zawadi toka kwa Mungu.Zawadi ambayo chimbuko lake ni ubatizo mmoja na
katika kushirkishana imani moja ya kanisa na maisha ya kisakramenti. Na Kanisa kama
familia kubwa , tumeungana wake kwa waume , wote pamoja katika Kristo, popote pale
tulipo
Papa aliendelea kusema, tunaweza kujiuliza ni kiasi gani sisi kama
Wakristu tunafurahia na kueleza na maisha yetu ya kila siku kushuhudia hayo, na
hasa katika maombi yetu, ukweli huu wa umoja na mshikamano wetu, katika usharika wa
Kanisa. Papa amehimiza Wakristu kutambua kwamba, dunia inahitaji shuhuda za
kimaisha kuonyesha mpango huu wa Mungu , katika mapatano, usharika, na amani ya
familia nzima ya binadamu.
Papa alieleza na kuhitimisha maelezo yake kwa
kumwomba Bwana, awawezeshe Wakristo wote duniani, kufanyakazi kwa ajili ya kuishinda
mivutano na migawanyiko iliyopo kati ya Wakristu, na wadumu katika umoja , kama alivyosema
Mtakatifu Paulo, “ kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili
mmoja na Roho mmoja kama mlivyoitwa katika tumiani moja la wito wenu. na kufurahia
mapatano kwa roho anayetengeneza utajiri wa wingi wenu mlio tofauti. taz. Efe 4:03