2013-09-25 15:09:46

Papa Francisiko :ubinadamu wa wahamiaji na wakimbizi haupaswi kuchezewa


Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya Wahamiaji, wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum, umeonya, ubinadamu wa wahamiaji na wakimbizi siyo vitunda vya kuchezewa katika bao za santaraji . Ujumbe huo wa Papa umetolewa siku ya Jumanne 24.09.13, kwa ajili ya adhimisho la 100 la Siku ya Dunia ya Wahamiaji na Wakimbizi , ambayo itakuwa tarehe 19 Januari. Maadhmisho hayo yataongozwa na Madambiu: wahamiaji na wakimbizi : kuelekea maisha bora ya baadaye.

Katika ujumbe huu, Papa analaani unyonyaji na madhulumu yanayofanywa kwa watu hawa wahamiaji na wakimbizi , na hivyo amezitaka nchi zote, kukabiliana na changamoto hii kwa moyo wa ubinadamu na uelewa wa kina kwa matatizo yanayomkumba mtu hadi kufikia maamuzi ya kuihama nchi yake . Na hivyo Papa ametoa wito kwa watu wote kufanya mabadiliko katika namna za kuwapokea watu hao wenye shinda. Wapokelewe kwa moyo wa ukarimu na upendo badala ya mitazamo ya chuki na hofu ya tamaduni kuchanganyika.

Papa Francisko anasema, nyakati hizi za utandawazi , zinatutaka tukabiliane na changamoto kwa mbinu mpya lakini zilizosimikwa katika haki na ukweli, ushirikiano wa kimataifa na roho ya mshikamano wa kina na huruma. Papa ametaja , tumaini la ulimwengu uliostaraabika na bora, linapaswa kuwaunganisha wanadamu wote, kwa hiyo ni muhimu kutenda kwa ajili ya manufaa ya wote. Papa ameongeza, inawezekana kuboresha hali iwapo tu zaidi ya yote, tunatoa angalisho makini kwa utu wa mtu, katiak utendaji wote wa maisha, yakiwemo masuala ya kiroho, kama nyenzo yenye uwezo wa kupitisha utamaduni wa kukutana na kukaribu.

Papa ameendelea kuwatetea wahamiaji na wakimbizi, kwamba ubinadamu wao, si goroli yakuchezewa lakini wanapaswa kutendewa kwa haki na usawa, kwa muono chanya kwamba, ni mtu mwenye nia njema za kutafuta mahali pa kusalimisha roho yake au kuinua maisha yake. Kuwashughulikia wahamaiji ni kushughulika na watu wa lika na kariba zote, tangu watoto, wanawake na wanaume ambao hulazimika kuacha nyumba zao kwa sababu mbalimbali.

Bahati mbaya, mara nyingi badala ya kupokelewa kwa upendo, mshikamano na ukarimu, huwa kinyume chake, kupingwa, kukataliwa, kubaguliwa, kunyonywa, kunyanyaswa na kulazimika kuendelea kusafiri wakipambana na mateso maumivu hata kifo. Kwa sababu mbalimbali za hali kukosa uhakika wa maisha, watu hawa hulazimika kuhama na hivyo huingia katika bila kutaka katika mfumo mbaya wa njia mbalimbali zinazo dharirisha utu wao na kuwa kafara wa utumwa mambo leo.

Papa Francisko akitazama hali hizo zote anasema, kanisa haliwezi kunyamalia madhulumu haya yanayo ingiza mamillioni ya watu katika hali ya umaskini na dhiki kubwa,watu ambao wamekimbia makwao wakiwa na matumaini mema kwa siku za usoni, lakini badala yake wanakumbana, maafa makubwa zaidi mara nyingi yenye kudhuru hadhi ya ubinadamu wao. Papa Francisko ameeleza na kunukuu ujumbe wa siku za nyuma wa Papa Benedict XVI, ambamo, alilia ushirikiano wa karibu bila ya kujali vikwazo vilivyopo kati ya nchi za asili wanakotoka na nchi waliko kimbilia, kama ilivyotajwa pia katika mwongozo wa kimataifa. " Hakuna nchi inayoweza kukabiliana na suala la wakimbizi peke yake , lakini ni suala linalohitaji ushirikiano na mshikamano wa karibu kwa mabara yote. .

Kisha ujumbe wa Papa, umetoa wito pia kwa mataifa , kuhamasisha uboreshaji wa hali ya uchumi nyumbani ,kupunguza kasi ya watu kutaka kwenda sehemu zingine kutauta malisho mazuri zaidi ya maisha. Uhamiaji na ukimbizi na uwe ni chaguo pekee kwa wale wanaotafuta amani, haki, usalama na heshima kamili katika ubinadamu wao. Pia mataifa yamehimizwa kutengeneza nafasi za kazi katika maeneo mahalia, kama hatua ya kuzuia mgawanyiko wa familia, ikiandamana na uhakika wa amani na utulivu.

Mwisho Papa Francisko, ametoa wito wa kuachana na chuki na hofu dhidiya wahamiaji na wakimbizi. Na ametoa ombi kwa vyombo vya habari na mawasiliano jamii, kuona wajibu wao mkubwa katika kuzuia ubaguzi na habari za uzushi , badala yake watoe habari sahihi juu ya malalamiko na makosa yanayo weza kufanyika, watoe maelezo kwa uaminifu, uadilifu, na moyo mkuu wa kuthamini utu wa binadamu. Na wajali kwamba, katika uso wa kila mtu, kuna mhuri wa uso wa Mungu, kigezo cha kwanza muhimu katika utendaji wenye ufanisi na tija, katika masuala yote ya kijamii, kikabila au kidini, izingatiwe kwamba hadhi ya mtu inatokana na yeye kuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Na hivyo wahamiaji wanakuwa sio tatizo katika kushughulikiwa, badala yake wanapaswa kupokewa na kukaribishwa kama ndugu.

Na kwamba kudra imetupa fursa ya kuchangia zaidi katika kujenga demokrasia kamili zaidi, umoja zaidi , kwa mujibu wa Injili . Uhamiaji - Papa anaandika, unaweza kuwa fursa kwa ajili ya uinjilishaji mpya . Kama ilivyokuwa kwa familia Takatifu ya Nazaret kukimbilia Misri, yanakuwa ni matakwa ya Papa pia, katika moyo ya Wahamiaji na Wakimbizi, kuwahakikishia kwamba, Mungu hatawaachi kamwe .








All the contents on this site are copyrighted ©.