cheni mapigano, na kuzingatia mazungumzo, nchi za maziwa makuu
Umoja wa mataifa unasema kwamba nchi zinazopakana naJamhuri ya Kidemokrasia ya watu
wa Congo zimekubali kutoingilia kati maslahi ya ndani ya nchi jirani zao kama njia
moja ya kutekeleza mkataba wa amani ulioafikiwa na nchi zilizomo kwenye maeneo ya
maziwa makuu mapema mwaka 2013.
Haya yamesemwa na Bi Mary Robinson, Mjumbe
maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Maziwa Makuu siku ya jumatatu kwenye kikao
na wawakilishi kutoka mataifa kumi ya eneo hilo, na wawakilishi wa kanda mbili za
bara Afrika. Amesema mjumbe huyo kwamba kazi iliyobaki ni kuhakikisha kwamba uamuzi
huo unatiliwa maanani na kutimizwa na kila nchi mwanachama wa maeneo hayo.
Migogoro
ya kivita inayoendelea hivi sasa nchini Congo ni kati ya wanamgambo wa M23 na majeshi
ya DRC. Ripoti kadhaa za uchunguzi wa Umoja wa Mataifa zinabainisha kwamba nchi ya
Rwanda imekuwa ikilisaidia kundi la waasi la M23 na kutumia fursa hiyo ili kuingia
nchini DRC na kujifaidisha na biashara ya madini kwenye eneo la mashariki la nchi
ya DRC.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban ki Moon ambaye amefanya
mkutano na mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini – Zuma, ameshtumu
vitendo vya kundi la M23 na makundi mengine ya wapiganaji wanaoendelea kusababisha
mateso mengi kwa wenyeji wa mashariki mwa DRC.
Bi. Robinson ameutaja mkutano
huo kuwa na mafanikio makubwa huku akisema baada ya mkutano huo aliwaona marais Paul
Kagame wa Rwanda na Joseph Kabila wa Congo wakiongea pamoja kwa namna ya kirafiki.