2013-09-23 15:53:46

Papa ameonya- bila kazi - utu wa mtu hudharirika.


Papa akutana na vijana wa Cagliari na kuonya kwamba, mtu bila kazi, utu wake hudharirika , na uzuzu kwa fedha hauwezi kudhibiti uchumi.
Jumapili Baba Mtakatifu Francisco akitembelea kisiwa cha Sardinia, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Cagliari, alisafiri kwa gari hadi uwanja wa Yenne ambako umati wa watu waliofika kumlaki wasiopungua 20 elfu wengi wao wakiwa katika lika la vijana.

Mahali hapo, ikiwa ni hotuba yake ya kwanza kwa wakazi wa kisiwa hicho , ambacho kimejeruhiwa na janga la ukosefu wa ajira, iliulenga ulimwengu wa kazi, akisema, hakuna kazi, hakuna heshima kwa utu wa mtu. Ni maneno yaliyotoka moyoni mwa Papa, akiwa pia ameguswa na shuhuda tatu zilizotolewa na alitolea sala kwa Bwana, ili awawezesha watu kupata nguvu za kupambana na kipindi kigumu cha kukaa bila ajira.

Papa alieleza na kulenga hasa kwa vijana wasio na ajira na pia watu wazima ambao ajira zao hufutwa kwa sababu mbalimbali, pia lwa waajiri na hata kwa wafanya biashara, wanaopambana na hali ngumu katika jitahidi za kusonga mbele. Katika mkutano huu , Papa mara kwa mara alishangiliwa kwa makofi na kilio cha " kazi , kazi kazi", mkutano ulio wekwa simanzi na shuhuda zilizotolewa na watu watatu, wakiwa mjasiria mali mmoja , mkulima mmoja na mfanyakazi kijana kibarua ambaye kwa sasa hana ajira. Wote waliweka tumaini lao kwa Papa, kama wana aminifu wanaotoa shida, hisia na siri zao kwa baba.

Papa Fracisko alisema, matokeo ya ukosefu wa kazi ni magumu, yasiyoweza kubebeka ndani ya familia. Na hii ni kti ya sababu kubwa , kwa mara nyingi, kutokuelewa mume na mke na matatizo mengi katika mahusiano na watoto wao, ni matokeo ya mgogoro huu mkubwa wa ukosefu wa ajira, jambo linalosikitisha watu wote. Nao waliokuwa wakimsikiliza Papa walitoa kilio chao kwa Papa wakisema, Papa Francisko wewe ni baba wa wote, usiliache kundi lako la kondoo kusambaratishwa na mbwa mwitu wanaotushambulia vikali kwa sabau ya kukosa matumaini katika maisha yetu wenyewe. usituache peke yetu.

Papa akiwa ameguswa na shuhuda na maneno ya watu, aliamua kutosoma hotuba yake aliyokuwa ameiandaa, badala yake aliikabidhi hotuba hiyo kwa Askofu Mkuu wa Cagliari , na kuendelea kuzungumzia juu ya ajira na hadhi ya kazi katika umuhimu wa uchumi wa binadamu. Papa alirejea kumbukumbu zake mwenyewe wakati baba yake alipohamishiwa Argentina , jiinsi alivyoishi kwa mateso ya kikosa kazi kutokana na kipeo kigumu cha uchumi katika miaka ya 1930.

Kwa uzoefu wake historia yake mwenyewe, Papa Francisko, ametaja njia pekee ya kujinasua na hali hizo ngumu ni jamii kujenga mshikamano na kuielewa changamoto hii ngumu kihistoria. Alibainisha kwamba, ziara zake mbili Italia, Lampedusa na sasa Sardinia , ameweza kuona mateso ya watu wengi, ambao wanajaribu hata bila ya kujali kwamba wana hatarisha maisha yao, utu wao, mkate wao, afya yao, wakiingia katika dunia ya wakimbizi bila kutazamia . Katika hayo aliyoyaona, Lampedusa, yanatoa changamoto kwa wenye navyo kuwapokea watu hawa walio katika mahangaiko ya kutafuta mkate wao wa kila siku.
Papa baada ya kukutana na vijana, watu maskini na wafungwa katika Kanisa Kuu la Cagliari,pia kwa muda mfupi alisamiana na kundi la wamonaki wa ndani. Kwa namna ya kipekee aliwatia moyo akisema, daima ninyi ni msaada wa Kanisa, msaada wa kiroho unaolidumisha kanisa katika utume wake, endeleeni na utume wenu kwa uaminifu, kwa kuwa Bwana amewaita ninyi katika huduma hii ya kuliombea kanisa kwa sala zenu kuu. Papa aliwabariki wote na kuwaomba wasiache kumkumbuka katika sala zao .








All the contents on this site are copyrighted ©.