Sista Angèlique ,mtawa wa Congo, ashinda tuzo ya Nansen2013.
Mtawa Sista Angèlique Namaika, Mkatoliki ambaye amekuwa kwa muda mrefu akisadia wanawake
wanaodhulumiwa kijinsia na Maaskari na waasi wa kikundi cha maasi cha LRA, katika
Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo , DRC, ametajwa kuwa kuwa mshindi wa tuzo ya Umoja
wa Mataifa ya Wakimbizi, kama kutambua juhudi zake, katika kusaidia wakimbizi.
Sista Angelique Namaika, amesaidia zaidi ya wanawake na wasichana 2,000 waliodhulumiwa
kinjisia na waasi wa LRA, katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Sista huyo anayejulikana
kwa wakimbizi wengi DRC, atapokea tuzo ya Nansen mwishoni mwa mwezi huu.
Tuzo
ya Wakimbizi ya Nansen, hutolewa kila mwaka na shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa
kwa waliotenda zaidi katika mazingira ya wakimbizi , na kwa mwaka huu, unhcr, imetambua
utendaji usiokuwa wa kawaida wa Sista Angelique, ambaye ameanzisha kituo katika mji
wa Dungu, Kaskazini Mashariki wma DRC, cha kutoa msaada kwa wanawake na waichana wanaodhulumika
kijinsia.
Kituo cha Dungu , kimeweza kubadili maisha ya wanawake wingi , kwa
kutoa elimu na mafunzo msingi katiak maisha yao . Tuzo ya Nansen, imetajwa kwa heshima
ya Fridtjof Nansen, mgunduzi mashuhuri , Mwanasayanasi na Mwanasiasa aliyekuwa Kamishena
wa kwanza wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Sista Angelique atapokea tuzo
yake Septemba 30, mjini Geneva. Na Octoba 2 , atakuwa Roma ambako atakutana na Papa
Francisko.